Miss Tourism World 2005- Africa

Miss Tourism  World 2005- Africa
Africa Tourism Promotion Centre

NGORONGORO CRATER

NGORONGORO CRATER
We Welcome Miss University Tourism World 2014 Contestants to Africa

THE GIDEON

BASATA YAPITISHA MABADILIKO MAKUBWA MISS UTALII TANZANIA,YAFUNGULIA SHINDANOBASATA YAIDHINISHA MABADILIKO MAKUBWA NA KIHISTORIA
YA MASHINDANO YA MISS UTALII TANZANIA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASTA),limeidhinisha mabadiliko yaliyo fanywa na bodi ya mashindano ya shindano la Miss Utalii Tanzania, mabadiliko hayo tunayoweza kuyaita ya kihistoria na mageuzi makubwa ya sanaa ya urembo nchini, yameidhinishwa sambamba na Baraza la sanaa kuruhusu kuanza kufanyika tena kwa mashindano haya ya pekee nchini,ambayo mbali ya bodi ya mashindano kuyasitishakwa muda , BASATA iliyafungia kwa muda usio julikana,kwa masharti ya kuitaka bodi ya mashindano haya kufanya maboresho ya kuimarisha mfumo wa mashindano na uongozi,baada ya fainali za mwaka 2013.

Kwa muda wa zaidi ya miaka mitano bodi tumekuwa tukifanya utafiti wa kisayansi na kimantiki kitaifa na kimataifa, utafiti ambao ulihusisha pia nchi mbalimbali zenye mafanikio makubwa katika sanaa ya urembo duniani, na kushirikisha taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa ,zikiwemo za Africa Tourism Promotion Centre na World Beauty Pageant Association, ili kupata mfumo bora na sahihi wa uongozi na mashindano haya adhimu nchini. Katika utafiti wetu,tulibaini haja ya shindano hili kuendeshwa kitaasisi badala ya kikundi cha mtu au watu, kupitia mpango mkakati maalum tulio upa jina la “Miss Tourism Tanzania at an Institution Level “ tuliona haja ya kuwa na mfumo rasmi wa uongozi (Organisation Structure) na mfumo rasmi wa shindano ( Pageant Structure).

Aidha katika utafiti wa faida na umuhimu wa shindano hili kwa jamii na taifa,tulibaini kuwa taifa linaweza kunufaika kupitia mashindano haya kwa kutangaza kimataifa Utalii,Utamaduni,Wanya mapori, Mazingira, Huduma za Misitu,Uwekezaji na kuhamasisha kitaifa Utalii wa ndani,Utalii wa Kitamaduni,Utalii wa Michezo,Utalii wa Mazingira na Utalii wa Mikutano,Vita dhidi ya Uwindaji na Uvuvi Haramu,Vita dhidi ya Uharibifu wa Mazingira na Misitu,vita dhidi ya tamaduni kongwe na potofu,vita dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia,wanawake na watoto. Hivyo kufuatia utafiti huo bodi imechukua hatua ya kuanzisha mfumo rasmi wa uongozi (Organisation Structure) na mfumo rasmi wa shindano (Pageant Structure),ambao umetoa mgawanyo wa madaraka ,majukumu na wajibu katika ngazi zote za mashindano,na kuwa na uwajibikaji wa pamoja wa kitaasisi (responsibility accountabilities),hivyo kuanzia sasa Miss Utalii Tanzania ni Taasisi ya rasmi ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania, iliyo sajiliwa kwa mujibu wa sheria zote za usajili za kitaifa na kimataifa.
Aidhapia katika kukabiliana na changamoto ya kutimiza wajibu wa shindano hili kwa Taifa, bodi imelibadili na kuwa shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania (Miss Tourism Tanzania International Pageant) kuanzia sasa. Ambapo shindano litakuwa na washiriki wa kitaifa wanao wakilisha kanda maalum nane (8) za Tanzania na washiriki wa kimataifa wawakilishi wan chi mbalimbali Duniani. Kanda za ngazi ya kitaifa za mashindano haya ,zimegawanywa kuzingatia Nyanja za kiutawala naza kiutalii, kanda hizo ni Miss Utalii Kanda ya Kusini, Kaskazini, Mashariki, Magharibi, Kati, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini, na Pwani. Hatua ya kulifanya shindano kuwa la kimataifa na mgawanyo wakikanda,unalenga kutoa fulsa kwa Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia washiriki watakao kuja kutoka nchi mbalimbali duniani,tofauti na awali ambapo Tanzania ilikuwa ikitegemea kujitangaza kupitia washindi wetu kwenda katika nchi nyingine kushiriki mashindano yanayo andaliwa au kufanika huko,,kinyume na ukweli kuwa wanafalsafa wote wa matukio ya kimaadhimishao ya kimataifa duniani,wanakubaliana kuwa nchi hunufaika pale tukio la kimaadhimisho linapo fanyika katika nchi husika,na sio kupeleka washiriki kushiriki katika nchi nyingine,na kukumbushakuwa washiriki huwa ni mabango ya matangazo ya nchi wenyeji.

 Lakini pia mgawanyo wa wmashindano kikanda utatoa fulsa kwa kanda na mikoa ilioyopokatika kanda husika kujitangaza kikanda na kitaifa,kupitia tukio moja kubwa la fainali za kanda zenye hadhi ya sio chini ya nyota nne hadi tano,tofauti na awali ambapo kila mkoa ulikuwa na fainali zake ambazo kwa sababu za gharama hazikuwezekana kufikia viwango vya nyota hata tatu,tofauti na sasa ambapo nguvu za wadhamini katika mikoa yote ya kanda ,wakiongozwa na serikali za mikoa husika wataunganisha nguvu kufanya fainali kubwa na za hadhi ya nyota hata tano, fainali ambazo zutarushwa LIVE kupitia Televisheni nchini na hata duniani kote,huku kanda na mikoa yote katika kanda ikijitangaza na kutangaza Vivutio vya Utalii ,fulsa za uwekezaji na kuonyesha na kudhihirisha hatua za maendeleo ambazo serikali katika mikoa yete imechukua na kufikia ikiwemo huduma za jamii,vita dhidi ya uwindaji haramu,uharibifu wa mazingira,uvuvi haramu n.k.
  Tunalishukuru na kulipongeaz kwa dhati baraza la sanaa la taifa ,kwa mchango wake wa hali na mali ,katika kipindi chote cha utafiti na upatikanaji wa kanuni mpya ya mashindano,muundo mpya wa uongozi na muundo mpya wa mashindano. Mchango ambao umelifanya shindano hili sasa kuwa bora na la mfano sio Tanzania tu bali Afrika mashariki ,Afrika na hata pande kadhaa za Dunia, lakini pia kutufanya tuandike historia nyingine katika tasnia ya mashindano ya urembo nchini ,ya kuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na shindano la kimataifa la Utalii,baada ya kuwa tumeandiak historia za awali za kuwa shindano la kwanza kabla na baada ya uhuru kutwaa taji la Urembo la Dunia ambapo Miss Utalii Tanzania 2004,Witness Manwingi alitwaa taji la Miss Tourism World 2005- Africa, na baadae kuwa shindano la kwanza nchini kuipa heshima Tanzania kuwa wenyeji wa shindano la Dunia 2006, na kuwa shindano pekee nchini ambalo katiak mashindano yote ya dunia na kimataifa tuliyo shiriki tumeshinda mataji ya dunia na kimataifa.
 Ujio mpya wa shindano hili wa Miss Tourism at an International Level ni fulsa nyingine kwa Taifa na jamii kitalii,kiuchumi na kijamii,na kipekee kiwekezaji, fainali za Taifa za kimataifa zimepangwa kushirikisha washiriki 100 ,toka nchi 100 duniani,, na washiriki 40 kutoka mikoa ya kanda 8 za Tanzania, fainali hizo zitarushwa LIVE duniani kote na kushudiwa na zaidi ya watazamaji 922,000,000 duniani kote. Kalenda rasmi ya mashindano haya,ambayo sasa tumekuwa na kalenda ya kudumu ya mashindano ,itatangazwa katiak mkutano na semina ya kimataifa ya waandishi na vyombo vya habari itakayo fanyika hivi karibuni. Hata hivyo kalenda ya kudumu ya mashindano haya , imelifanya shindano hili kuwa sehemu ya maazimisho ya sherehe za Taifa za suhuru wa Tanzania kila mwaka,na kuileta Dunia kuwa sehemu ya sherehe za Uhuru wa Tanzania kila mwaka, huku wakitangaza Utalii,uwekezaji,huduma za misitu,wanyama pori na mazingira ya Tanzania duniani kote.


Malengo ya shindano hili pia  yameborehwa  ili  kukidhi matakwa  ya kuwa shindano la kimataifa, bila kuathili tamaduni na mila njema  za Tanzania na Afrika. Malengo mahususi ya mashindano haya ni kuunga mkono juhudi zaserikali na mamlaka zake ,kwa kutafsiri kwa vitendo sera za Taifa  za Utalii, Utamaduni, Michezo, Wanyama pori, Misitu, Uwekezaji, Mazingira, Biashara, Viwanda,wanawake , Jinsia  na Watoto kitaifa na kimataifa.

Mashindano ya kimataifa ya Miss Utalii Tanzania (Miss Tourism Tanzania International Pageant ), ni tafsiri ya vitendo ya sera za Taifa za Utalii,Uwekezaji,Mazingira,Wanyamapori,Misitu,Mambo ya Nje na Maendeleo ya Jamii , lakini pia ni uungaji mkono kwa vitendo wa juhudi na hatua za serikali ya awamu ya tano ,chini ya uongozi madhubudi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mheshimiwa John Pombe Magufuli, ambapo tumeshudia sekta ya Utalii ikipewa uzito stahiki na kuchukua sura mpya kitaifa na kimataifa,. Nasi tunaamini  wakati sasa umefika teana wakati sahihi kwa kila mmoja wetu kuunga mkono na kushiriki kwa namna moja au nyingine katika kukuza Utalii,ambao ni kati ya sekta muhimu katika uchumi wa taifa letu,ambapo sasa utana changia zaidi ya 25% ya pato la fedha za kigeni,na 17% ya pato la Taifa ,lakini sekta ya Utalii ina changia 12% ya ajira zote Duniani, ikiwa na maana kuwa katika kila ajira 100 ,basi 12 zimetokana na utalii.No comments: