MIKIDADI
MAHMOUD MWENYEKITI WA BODI MISS UTALII TANZANIA
Bodi
ya Miss Tourism Tanzania Organisation,yenye dhima ya kikomo ya kuaandaa na
kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania ,imemteua Ndugu Mikidadi Mahamoud
kuwa mwenyeketi ya bodi ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania. Uteuzi huo
utakuwa ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 1-10-2012.
Akuthibitisha
uteuzi huo, Gideon Chipungahelo,Rais wa Miss Utalii Tanzania, hatua hii ni moja
ya utekelezaji mpango mkakaeu wa miaka mitano wa kuimalisha mashindano na mfumo
wa uongozi wa mashindano haya. Ambapo sasa tunakuwa na bodi ya mashindano na
bodi ya taifa ya ushauri ambayo itajumuisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii
na serikali. Tayali tumeiandikia serikali kupitia Bodi ya Utalii Tanzania, tukiiomba
kuwa na wajumbe katika bodi ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania, ambapo kutakuwa
na wajumbe pia kutika katika mamlaka mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Mazingira,
Elimu, Afya, Uwekezaji, Jinsia na asasi za kupambana na umasikini kupitia
utalii na utamaduni. Mamlaka na Asasi hizo ni pamoja na Mamlaka za Hifadhi za
Taifa, Bodi ya Utalii, Bodi ya Madini, Kurugenzi ya Utamaduni, Kurugenzi ya
Utalii, Kituo cha uwekezaji Tanzania, Kurugenzi ya Mazingira na Tanzania
Association for Tour operators.
Lengo
la kufanyia mabadiliko ya mfumo wa uongozi na uendeshaji ni pamoja na kupanua
wigo wa ushiriki wa mamlaka za umma na za binafsi katika uendeshaji wa
mashindano haya,ambayo hakika ni alama ya urithi wa taifa na muhimu sana katika
kuhamasisha ukuaji wa utalii wa Tanzania na kuhamasisha Utalii wa ndani,utalii
wa kitamaduni,utumiaji wa bidhaa za kitanzania,utalii wa michezo,utalii wa
mikitano,pia kuhamasisha vita dhidi ya uharibifu wa mazingira,uwundaji
haramu,uvuvi haramu,tamaduni kongwe na potofu,vita dhidi ya ujinga,umasikini na
maradhi.
Bodi
katika kumteua Ndugu Mikidadi Mahamoud kuwa mwenyekiti wa bodi,imezingatia
busara,hekima na uzoefu wake mkubwa katika katika Nyanja za kitaifa na
kimataifa za michezo,utangazaji,uhamasishaji na ushiriki wake mkubwa katika
kufanikisha matukio makubwa ya Kitaifa na kimataifa.Tunaamini uzoefu na uimara
wake mkubwa katika uongozi wa kada mbalimbali utakuwa ni muhimili na chachu
mpya ya mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania na kuchangia katika ukuaji wa
sekta ya Utalii nchini. Mikidadi Mahaumod ambaye amewahi kufanya kazi katika
vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa na kimataifa, kwa sasa ni Mkurugenzi
wa Redio uhuru ya jijini.
Aidha
fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania kuanzia mwaka zitakuwa zikifanyika
mwezi Didemba 2012 sambamba na sherehe za Uhuru wa Tanzania . Ambapo kwa mwaka
huu, karibu mikoa yote imekamilisha fainali zake, kasoro mikoa ya
Arusha,Dodoma,Kulimanjaro,Mara na Iringa ambayo warembo wapo kambini
wakiendelea na mazoezi na itakuwa imekamilisha fainali hizo kabla ya Novemba 15
,2012.
No comments:
Post a Comment