Raisi wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo akimkaribisha Mratibu wa masoko wa Chuo kikuu cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.
Mratibu Mkuu wa Masoko wa School of Journalism and Mass Communication Bi . Sophia akizungumza Jambo Na washiriki wa Miss Utalii Tanzanaia Taifa 2012/13
Mratibu wa Masoko wa Chuo kikuu cha waandishi wa Habari akisikilaza kwa umakini salamu za Shukurani, Muda mchache baada ya yeye Kumaliza kuongea.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa
Masoko wa Chuo Hicho Bi Sophia Ndibalema.
Chuo Kikuu cha Waandishi wa kimewapongeza Miss Utalii
Tanzania Taifa 2012/13 kwa elimu walizo nazo na kuwasihi watumie elimu zao
kutangaza utalii wa Tanzania Jambo ambalo lina manufaa makubwa kwa jamii ya
Watanzania Akizungumza na washiriki hao Kijitonyama Jijini Dar es salaam, Mratibu
wa masoko wa chuo hicho
ndugu Sophia Ndibalema aliwataka kutumia Fulsa ya kuwa
warembo hasa utalii kwa kujitaftia nafasi zaidi za elimu ya juu kwa
manufaa yao Jamii na Taifa kwa ujumla, alisema nafasi zipo wazi kwa wale wenye
kuhitaji na wenye sifa za kujiunga chuoni hapo kwa nafasi ya Cheti, Diploma na
Shahada, alisema amefurahishwa na muonekano wa asili na mavazi ya heshima kwa
washiriki hao hivyo kuondoa dhana kuwa washiriki wa urembo kuwa ni wale
wanaovaa mavazi yenye Kudhalilisha jamii
hii inathibitisha kuwa Miss Utalii ni Zaidi ya Mashindano Mengine na ni Alama
ya Urithi wa Taifa na kielelezo cha mwanamke au Binti wa Kitanzania
No comments:
Post a Comment