Serikali yawapiga Msasa Washiriki Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania 2012/13
Serikali kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii,imeendesha semina
ya washiriki wa Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania 2012/13 iliyo fanyika leo
Katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao makuu ya Bodi ya utalii Tanzania.
Semina hiyo ambayo ilifunguliwa na Kaimu mkurugenzi Mtendaji
wa Bodi ya Utalii Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo
Ndugu Devotha Mdachi, imeandaliwa na Bodi ya Utalii kwa lengo la Kuwapiga msasa
washiriki hao kabla ya fainali ya Taifa itakayo fanyika 17.03.2013 katika
ukumbi wa Dar Live.
Akifungua Semina hiyo Ndugu Devotha mdachi pamoja na
kuwakaribisha washiriki wote makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania aliwaasa
washiriki hao kujifunza na kuvielewa kwa kina vivutio vya utalii Tanzania ili
wale watakao shinda na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano
ya Dunia waweze kuitangaza vema Utalii wa Tanzania na nchi kwa Ujumla.
Aliwakumbusha pia wao kama warembo wa utalii wanalo jukumu la kuunda mkono
juhudi za Serikali kuhamasisha utalii wa Ndani lakini pia jukumu la kutangaza
vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa na Kimataifa. Aliendelea kuwaasa pia
wao kama warembo wa utalii wanapaswa kujivunia utanzania na Maliasili zake huku
wakidumisha Mila na Utamaduni wa Tanzania na kwamba siku zote wanatakiwa kuwa
na nidhamu ya hali ya juu na mfano wa kuigwa katika jamii kwa maana warembo wa
utalii ni alama ya Urithi wa Taifa na kielelezo cha Mwanamke wa Kitanzania.
Aliwakumbusha wale watakao shinda kwenda kutetea Mataji ya Dunia ambayo Miss
Utalii Tanzania wanashikiria .
Nae mtoa mada Mkuu katika semina hiyo Ndugu Deogratias
Malogo ambaye ni Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa Bodi ya Utalii Tanzania
aliwafahimisha warembo wa Miss Utalii Tanzania wa Fainali za Taifa 2012/13 kuwa
secta ya utalii ni secta muhimu katika Uchumi na kuchangia pato la Taifa kila
mwaka. Alisema Secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 20 ya pato la
tTaifa kila mwaka na zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa la fedha za kigeni
kila Mwaka. Alisema Kidunia secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 12 ya
ajira zote Duniani.
Warembo hao walifundishwa Historia ya utalii Tanzania .
Walifundishwa vivutio vya utalii Tanzania, Mbinu za kutangaza utalii wa
Tanzania Kitaifa na Kimataifa, lakini aliwaelezea pia jitihada ambazo serikali
kupitia bodi ya taifa ya utalii na Mamlaka nyengine za utalii nchini imekuwa
ikifanya katika kukuza secta ya utalii na kutangaza vivutio vya utalii kitaifa
na Kimataifa. Ndugu Malogo aliwaelezea juu ya umuhimu wa utalii wa ndani katika
kukuza na kuchangia pato la utalii la Taifa na kwamba wao kama warembo wa
utalii ni sehemu muhimu katika kukuza na kuendeleza secta ya Utalii Tanzania
kwani wao ni kioo cha jamii na mfano wa kuigwa kitabia Mwenendo Muonekano na
Hulka. Aliwatakia kila laheri wale watakao shinda katika fainali hizo za Taifa
kwenda kuwa mabarozi bora wa Tanzania katika mashindano ya Dunia watakayo
kwenda Kushiriki.
Nae Rais wa Miss Utalii Tanzania alitoa shukurani na Pongezi
kwa Bodi ya Utalii Tanzania kwa juhudi kubwa wanazo fanya ya kuinua na
kuendeleza secta ya utalii nchini. Alipongeza na kushukuru pia hatua ya bodi ya
utalii, kwa kuendesha Semina Maalum kwa washiriki wa fainali za Taifa za Miss
Utalii Tanzania 2012/13 na kusema kwamba semina hii itakuwa ni Dira na ufunguo
kwa Miss Utalii Tanzania wa kutwaa mataji zaidi ya Dunia katika mashindano yote
watakayo shiriki na pia katika kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani Kitaifa
na Kimataifa.
Asanteni
Fredy Tony Njeje
Marketing and Public Relation Miss Utalii Tanzania.
No comments:
Post a Comment