Wakati maandalizi ya Fainali za Taifa za kumpata Miss Utalii
Tanzania 2012/13 yakiwa yanaendelea kwa kasi kubwa, Bodi ya Utalii Tanzania itaendesha Semina Maalum ya
Mafunzo ya Utalii kwa washiriki wote walioko kambini Ikondolo Lodge Kibamba
wakijiandaa na Fainali za Taifa zitakazo fanyika Mwishoni mwa wiki ijayo Jijini
Dae es salaam.
Akithibitisha taarifa hizo
kwa waandishi wa Habari Raisi
wa Kamati ya Mashindano hayo Erasto G.
Chipungahelo alisema kuwa Semina hiyo
maalum itakayo endeshwa na Bodi yaUtalii Tanzania itafanyika katika Ukumbi wa
Bodi ya Utalii uliyopo katika ofisi za Bodi ya Utalii jingo la IPS Dar es
salaamsiku ya Alhamisi Tarehe 7.03.2013 kuanzia saa Tatu asubuhi na
kuwashirikisha zaidi ya Warembo 40 wakiwakirisha Mikoa yote ya Tanzania Bara ,
Kanda maalum za Vyuo vikuu na Zanzibar. Watoa mada wakuu katika semina hiyo, itakuwa
ni wataalam walio bobea katika secta ya utalii na masoko ya utalii kutoka Bodi
ya Taifa ya Utalii(Tanzania Tourist Board).
Kwa niaba na kamati ya Miss Utalii Tanzania, Ninatoa
shukurani za pekee kwa Serikali na Bodi nzima ya Utalii kwa kuendesha semina
hii muhimu kwa washiriki wa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania ambapo
washindi wa kwanza mpaka wa Tano watawakirisha Tanzania katika mashindano
mbalimbali ya utalii ya Dunia. Yakiwemo ya Miss Tourism World, International
Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation World , Miss Tourism university
World na Miss Heritage World. Yatakayo fanyika katika nchi mbalimbali kuanzia
mwezi wa nne mwaka huu.
Hii ni fulsa ya pekee kwa washiriki na washindi watakao
patikana katika fainali za Taifa kuweza kujua na kujifunza juu ya utalii
Tanzania, mbinu na mikakati ya kutangaza vivutio vya kitalii kitaifa na
kimataifa, hivyo kutusaidia kutimiza ndoto na malengo yetu ya miaka mitano ya
kutwaa Mataji matatu ya Dunia mwaka 2013.
Maandalizi katika kambi ya warembo yanaendelea vizuri ,
ushindani ni mkubwa ari na dhamira ya kila Mrembo kulinda hadhi na Heshima ya
Mkoa wake kwa kutwaa taji la Taifa ni kubwa.
Chipungahelo aliongeza kwamba, ili kuthibitisha hayo,
anaomba watanzania wote wakazi wz Dar es salaam na Mikoa ya Jirani, wajitokeze
kwa wingi siku ya ya Jumamosi Tar 9.03.2013 usiku katika ukumbi wa Dar Live
Mbagala kushuhudia warembo hawa wakipanda jukwaani kuwania Tuzo mbalimbali za
Vipaji na Utamaduni. Ambapo mbali na kupita jukwaani na mavazi mbalimbali
washiriki wote pia watashindana kucheza na kuimba nyimbo za Asili za Mikoa
wanayo wakilisha. Na hili litakuwa ni tukio la kihistoria la Utalii, Urembo na
Utamaduni kuwahi kufanyika hapa Tanzania kabla na Baada ya Uhuru.
Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu
Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca
Cola Kwanza, VAM General Suppries Limited,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro
Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata
Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA )
www.misstourismorganisation.blogspot.com
No comments:
Post a Comment