Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko (katikati) ,Matron Hilda Mwinyi (Kulia), na Mratibu wa kamati ya maandalizi Kessy Salum Mbasha (Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013, alipo kwenda kukagua kambi na kuzungumza na warembo hao Jana katika hoteli ya Mwambani Tanga Beach
Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko (katikati), Mjumbe wa Kamati ya maandalizi na Mbunifu wa Mavazi ya warembo Aisha Khoja toka Kokoriko Designer, (Kulia), na Mbunifu wa mavazi Edina Katarai ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi (Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013, alipo kwenda kukagua kambi na kuzungumza na warembo hao Jana katika hoteli ya Mwambani Tanga Beach.
Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko (katikati), Mjumbe wa Kamati ya maandalizi na Mbunifu wa Mavazi ya warembo Aisha Khoja toka Kokoriko Designer, (Kulia), na Mratibu msaidizi wa kamati ya maandalizi Mfaume Silai Luoga (Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013, alipo kwenda kukagua kambi na kuzungumza na warembo hao Jana katika hoteli ya Mwambani Tanga Beach.
****************
Wakati Maandalizi ya fainali
za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013 yanaendelea kwa kasi katika hoteli ya
kitalii ya Mwambani iliyopo katika ufukwe wa Tanga, huku kila Mrembo akijifua
vikali, Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Tanga Ndugu Peter Semfukwe ametembelea
kambini hapo, kujionea yeye mwenyewe warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 ambao
wanajiandaa na Fainali hizo za Taifa zitakazo fanyika wiki Ijayo,kasha
alizungumza nao na kuwakaribisha mkoani Tanga.
Afisa Utamaduni alisema
kuwa amefurahi kukutana na warembo wote wakiwa katika Afya Njema, Mvuto
na kila mmoja kuonekana ndiye atakaye twaa taji hilo la Miss Utalii Tanzania
2013, pia ameipongeza kamati ya maandalizi kwa juhudi na jitihada kubwa za
kuandaa mashindano hayo ambayo dhima yake ni kuutangaza utalii wa ndani pamoja
na utamaduni wa Mtanzania. Aliongeza
kuwa anaahidi ushirikiano mkubwa wa hali
na mali wakati wa maandalizi mpaka mwisho wa mashindano hayo.
Akizungumza na Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Miss Utalii Tanzania , Afisa Utamaduni aliwaasa warembo hao wawe na heshima, adabu, na pia wawe ni mfano bora wa kuigwa katika jamii ikiwa ni warembo hao kuwa mstari wa mbele katika kushiriki, kutangaza Utalii na Utamaduni wa Mtanzania.
Mpaka sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini ,wanajiandaa vizuri kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
Akizungumzia, juu ya maendeleo ya
kambi, Fredy Njeje, alisema kuwa baada ya kukwamishwa na wadhamini walio toa
ahadi hewa, wamelazimika kuhamishia shindano hilo mkoani Tanga,baada ya
kuvutiwa na mwamko wa wafanya biashara na makampuni ya Jiji la Tanga wa kuwa na
uwezo wa kudhamini matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa.
Tunakabiliwa na changamoto ya
warembo wengi kuwa wapya katika kambi yetu,baada ya wale waliokuwako kambini
kabla ya kambi kuahirishwa kushindwa kurudi kambini kwa sababu
mbalimbali,zikiwemo za kimasomo na wengine kukata tama baada ya kuahirisha.
Hata hivyo tayali nafsi zao zimechukuliwa na washindi wa pili wa mikoa yote
ambayo warembo wake wameshindwa kurudi kambini, na tayali warembo 30 wameripoti
kambini na tunategemea wengine 10 kuripoti kambini wakati wowote ili kufikisha
idadi ya warembo 40 wata kao panda jukwaani. Tumejiandaa na tunapata
ushirikiano mkubwa kwa serikali ya mkoa nay a Jiji la Tanga, hivyo
kutuhakikishia kuwa tarehe itakayo pangwa sasa haitabadilika tena wala
kuahirishwa. Tarehe kamili ya shindano itatangazwa kesho na mwenyekiti wa
kamati ya maandalizi ambaye pia ni Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga.
Washindi
wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano
mbalimbali ya Dunia na nchi yatakako fanyika katika mabano International Miss Tourism World
(Marekani), Miss Tourism United Nation (Mexico), Miss Heritage World
(Tunasubiri Taarifa), Miss Tourism University World(Tanzania), Miss Globe
International (Uturuki), Miss Tourism World ( Equatorial Guinea ), Miss Freedom
Of The World ( Kosovo) , na Miss Tourism United Nation (Nigeria) n.k
Wakati
huohuo, katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya Fainali za taifa, za mashindano
hayo ambapo mkoa wa Tanga unakuwa wenyeji kwa mara ya kwanza yanafanyika kwa
ubora na hayakwami, kamati ya maandalizi ya kimkoa umeundwa ambayo mwenyekiti
wake ni Peter Semfuko Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga. Miss Utalii Tanzania
,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo
ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss
Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism
Model
Of The World 2008-Personality, Miss Africa 2006 – 1ST Runner Up n.k
Asante,
Fredy
Njeje
Mkurugenzi
wa Masoko na Mahusiano ya Umma
1 comment:
This helps business managers to determine what the general
public thinks about their products or services. Listening to Internet radio is
a breeze for anyone who's familiar with the World Wide Web. You can see if any of your Facebook friends are listening by clicking on the Facebook link on the bottom right.
Here is my site - Mouse Click The Next Webpage
Post a Comment