MISS UTALII TANZANIA KWENDA
MISS TOURISM WORLD 2013
MISS TOURISM WORLD 2013
Miss
Utalii Tanzania 2013, Hadija Mswaga, anaondoka nchini kuelekea Equatorial Guinea kuwakilisha Tanzania katika Mashindano ya
Dunia ya Miss Tourism World 2013. Atasafiri kwa ndege ya shirika la ndege la
Ethiopian Airline.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 |
Katika
mshindano hayo yanayo shirikisha nchi 126 duniani kote, na kuonyeshwa LIVE
katika Televisheni Duniani kote, Miss Utalii Tanzania 2013, anabeba ujumbe wa
kutangaza Hifadhi ya Ngorongoro Crater kama moja ya maajabu ya Dunia Afrika.
Akitoa sababu za kuibiba Hifadhi ya ngorongoro katika mashindano hayo, Hadija
Mswaga, alisema kuwa mbali ya hifadhi hiyo kuwa ni ya kipekee duniani, lakini
ndiyo hifadhi ambayo chimbuko la binadamu wa kwanza kuishi duniani, pia hifadhi
hiyo ndio kitovu cha hifadhi ya faru nchini, mbali ya kuwa ndiyo hifadhi pekee
duniani ambako binadamu na wanyama wanaishi na kushirikiana maisha ya kila siku
bila ya kudhuriana. Wakati
sasa umefika tena wakati sahihi kwa hifadhi ya ngorongoro kuwa hifadhi kiongozi
kwa umaarufu ,pato la utalii na kutembelewa na watalii wengi zaidi duniani
alisema hadija.
No comments:
Post a Comment