MISS TOURISM CONTESTANT |
Afrika ya Mashariki imepewa heshima
ya kuwa wenyeji wa Tamasha la Dunia la Utalii,Michezo na Utamaduni (World Great
Safari Tour 20114/15). Tamasha hilo ambalo litashirikisha zaidi ya nchi 120,litajumuisha
Safari za kutembelea na kupiga picha za Video,Magazeti,Televisheni na Majarida
ya kitaifa na kimataifa katika Vivutio vya Utalii,litajumuisha pia mashindano
ya Dunia ya Mibio za Nyika ya kilomita 21 ya Ant Poaching International
Marathon ,ya mita 10,000 ya National Parks International Marathon 2014/15 na ya
mita 5,000 ya Wildlife International Marathon 2014/15, ambapo kwa upande wa
utamaduni na burudani litajumuisha Ngoma za Asili na Mashindano ya urembo ya
Dunia ya Miss Tourism University World 2014/15.Pia tamasha hili litajumuisha
mashindano yam bio za magari na baisikeli ya Dunia.
Aidha Tamasha hilo
litajumuisha Utoaji wa Duzo za Dunia za Utalii za “World Tourism awards 2014/15
na mashindano ya mchezo wa masubwi.
Tamashahilo litashirikisha
washiriki wanamichezo,warembo,wasanii, wanamitindo wa kimataifa na watu
mashuhuri na maarufu Duniani, wakiwemo wanadiplomasia na wana harakati wa kimataifa
wa haki za Wanyamapori na mazingira kutoka nchi mbalimbali Duniani.Waandishi wa Vyombo vya habari vya
kimataifa na kitaifa vya Televisheni ,Magazeti,Majarida ,Tovuti na Mitandao ya
kijamii, watakuwa ni miongoni mwa washiriki wa Tamasha hilo,la kihistoria
kuwahi kufanyika barani Afrika, hususani Afrika ya Mashariki. Likiwa
linaandaliwa na Kampuni ya Africa Tourism Promotion Centre, Tamasha la World
Great Safari Tour 2014/15, lita onyeshwa LIVE uniani kote kupitia Televisheni
na Tovuti na Mitandandao ya Internet.
MISS TOURISM CONTESTANTS |
Hii ni fulsa nyingine ya pekee kwa
nchi ya Afrika ya Mashariki ,itakayo shinda Uteuzi wa kuwa wenyeji wakuu wa
Tamasha hilo,kuonyesha duniani kote vivutio vyake vya utalii,mianya na fulsa za
uwekezaji , lakini pia hii itakuwa ni fulsa kwa nchi hiyo kuonyesha Dunia
juhudi za serikali yake,asasi binafsi na za umma katika kupambana na ujangili
,hususani uwindaji haramu,uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira,na kuvutia
misaada na udhamini wa kitaifa na kimataifa katika kupambana na
Ujangili,uharibifu wa mazingira na uwindaji haramu kwa ujumla.Nchi wenyeji itapata fulsa na
heshima ya kuidhibitishia Dunia kuwa ni nchi yenye vivutio vya utalii,ni nchi
yenye amani na salama kwa watalii na wawekezaji. Pia kuithibitishia Dunia kuwa
ni nchi yenye uwezo na hadhi ya kuwa wenyeji wa matukio makubwa ya Dunia na
mengine ya kimataifa, kimiundombinu, usalama, nguvu kazi na hata ukarimu na
mahusiano ya kitaifa na kimataifa.
Mchakato wa kupata nchi
wenyeji wa Tamasha hili ,huanzia ngaziya
kushindanisha mabara yote ya Dunia, ambapo bara la Afrika lilishinda, na hatua
ya pili huwa ni kushindanisha kanda za bara husika ambapo Afrika ya Mashariki
ilishinda. Hatua inayo fuatia sasa ni uteuzi wan chi ambayo itakuwa ndio
wenyeji wakuu miongoni mwa nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki. Mazungumzu
yapo katika hatua nzuri na serikali na baadhi ya asasi binafsi za nchi za
Afrika ya Mashariki , na yatakapo kamilika tutaitangazia Dunia nchi iliyo
shinda katika mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari,utakao fanyika
katikla nchi hiyo husika.Katika uteuzi huo,tunazingatia
vigezo mbalimbali, vikiwemo vya amani,ulinzi na usalama wa nchi husika, utayari
wa nchi na serikali ya nchi husika wa kushirikiana kujitangaza kitaifa na
kimataifa, uwepo na uhalisia wa vivutio vya kitalii katika nchi husika,uwepo wa
juhudi na nia ya dhati ya nchi husika katika kupiga vita Ujangili,Uharibifu wa
Mazingira na uwindaji haramu kwa ujumla. Na kubwa zaidi ni uwepo wa sera ya
utalii ambayo inatambua kuwa utalii ni moja ya sekta madhubuti katika kukuza
uchumi wa Taifa na kupiga vita umasikini.
MISS TOURISM |
Hili ni tukio kubwa Duniani,ambalo
litashirikisha washiriki zaidi ya 1500 kutoka zaidi ya nchi 120 duniani, wakitangaza
utalii,utamaduni,michezo,huku wakipiga picha za video na Televesheni katika
hifadhi za Taifa,Mapori ya akiba, na vivutio vingine vya utalii katika nchi
wenyeji. Tukio hili kuu la kitalii Duniani litaonyeshwa LIVE duniani kote
kupitia Televisheni na mitandao ya Internet , na kushudiwa na zaidi ya
watazamaji Bilioni 1.5 duniani kote,huku waandishi wa habari wa kimataifa za
Televisheni,Redio na Magazeti wakiambatana na washiriki kutoka nchi mbalimbali
duniani.
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Makamu wa Rais Dunia – World Great
Safari Tour/Africa Tourism Promotion Centre
No comments:
Post a Comment