ANCHI
AFRICA MASHARIKI ZACHUANA UENYEJI TAMASHA LA UTALII LA DUNIA LA “WORLD GREAT
SAFARI TOUR 2014/2015”
Miss Tourism Tanzania 2005 |
Bodi ya Africa Tourism Promotion
Centre, waandaaji wenye dhima ya kikomo ya kuratibu na kuendesha tamasha la
Dunia la Utalii la “WORLD GREAT SAFARITOUR” 2014/2015 ,wakishirikiana na
kampuni ya Miss Tourism Tanzania Beauty Pageant Limited, ipo mbioni kukamilisha
mchakato wa kuteua nchi itakayo kuwa wenyeji wa tamasha hilo la kimataifa la
Utalii.
Miss Tourism World 2005 |
Katika hatua ya mwanzo mchakato huo
ulishindanisha mabara yote ya dunia,yakiwemo ya Asia,Ulaya,Marekani,Rusia, Asia,India na
Afrika , ambapo bara la Afrika liliyabwaga mabara mengine na kuteuliwa kuwa
wenyeji wa Tamasha hilo la Dunia. Katika hatua ya pili waandaaji
walishindanisha kanda za bara la Afrika ,zikiwemo kanda za Afrika
Magharibi,Afrika Kaskazini,Afrika ya Kati, na Kusini ambapo Afrika Mashariki
iliibuka washindi na kupewa heshima ya kuwa
wenyeji wa Tamasha hilo la Dunia la World Great Safari Tour 2014/2015.
Miss Tourism 2998
Katika hatua ya mwisho ya mchakato wa kupata wenyeji wa tamasha hilo, nchi za kanda ya Afrika ya Mashariki zinashindanishwa ambapo nchi itakayo shinda kati ya Kenya,Burundi,Rwanda,Tanzania na Uganda ndiyo itakayo pewa heshima ya kuwa wenyeji wa Tamasha hilo kubwa la kimataifa la Utalii Duniani.
Miss Tourism World 2005 |
Miss Tourism 2005 |
Miss Tourism 2005 |
Tamasha hilo ambalo litaonyeshwa
moja kwa moja (LIVE) duniani kote kupitia Televisheni na Mitandao ya Internet ,
litajumuisha zaidi ya nchi 120, na kuangaliwa LIVE na zaidi ya watazamaji
1bilioni wa Telvisheni na Mitandao ya Interneti.
Tamasha hilo Kuu la Utalii la Dunia “World Great Safari Tour 2014/2015” litajumuisha mashindano ya dunia ya Miss Tourism University World 2014/15,Mbio za nyika za Dunia za Ant Poaching International Marathon, Wild Life International Marathon, National Parks International Marathon, Mbio za kimataifa za Magari na Baisikeli na tuzo za Dunia za Utalii “World Tourism Awaards 2014/2015”.
MissTourism 2006 |
Miss Tourism 2007 |
Vigezo ambavyo Bodi intazingatia katika
kuteua nchi wenyeji ni pamoja na Uwepo wa Vivutio vya Utalii katika nchi
husika, Dhamila na juhudi za nchi husika kutangaza utalii wake kimataifa na
kitaifa, Haja,Juhudi,Utayali na dhamira ya kupiga vita Ujangili ,Uharibifu wa
Mazingira ya nchi husika katika nchi husika, lakini kubwa zaidi ni
Amani,Usalama,Fulsa za Uwekezaji wa kitalii na utengamano wa kimataifa na
kitaifa wan chi husika. Pia nchi kuwa na uwezo wa kuwa wenyeji wa tukio au
tamasha la kimataifa hapa suala la miundombinu ya mawasiliano,usafiri,mahoteli,rasilimali
watu,utayari wa serikali na mamlaka zake za utalii,mazingira katika
kushirikiana na waandaaji na mahitaji mengine ya msingi vinazingatiwa.
Miss Tourism 2009
Asante,
Gideon Erasto Chipungahelo
Makamu wa Rais Dunia Africa Tourism
Promotion Centre/ Miss Tourism Organisation
No comments:
Post a Comment