Taarifa Kwa Vyobo Vya Habari Taraehe 5-8-2017
BODI YA MASHINDANO YA MISS UTALII TANZANIA YATEKELEZA MAAGIZO YA
BASATA – CHINI YA AFRICA TOURISM PROMOTION CENTRE
Bodi ya
wakurugenzi ya kapuni ya Miss Tourism Tanzania Organisation yenye dhima ya kikomo ya kuandaa
ashindano ya Miss Utalii Tanzania na ya Miss Tourism University World, Miss
Tourism Tanzania imeikaimisha
kampuni ya Africa Tourism Promotion Centre , kuratibu ashindano ya Miss Utalii Tanzania , ambayo yalisitishwa na Bodi hiyo
na BASATA mwaka 2013.
kwa mujibu wa
Taarifa iliyo tolewa na Taasisi hiyo na kusainiwa na mwenyekiti mtendaji
wa Africa Tourism Promotion Centre ambaye pia ni rais wa mashindano hayo, amesema kuwa hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa
aelekezo ya BASATA na Bodi ya mashindano ilikuiarisha uongozi
na mfumo wa mashindano ili kuyaboresha kwa viwango vya kimataifa.
Pamoja
na mambo mengine African Tourism Promotion Centre
,itasimamia mashindano hayo kwa mfumo mpya ambao
umepitishwa na bodi,ikiwemo mashindano kufanyika kuanzia ngazi za kanda
badala ya wilaya na mikoa, ili kuimalisha ubora na upatikanaji
wa washiriki wenye viwango.
Mashindano ya Miss
Utalii Tanzania tofauti na mashindano mengine
chini yamekuwa ndiyo pekee yakiiletea
heshima na kuitangaza
Tanzania kwa kushinda mataji ya kimataifa ndangu kuanzishwa kwake
nchini mwaka 2005. Huku yakiwa ni ya kwanza katika historia ya Tanzania
kutwaa taji la Dunia, na pia kuipa heshima Tanzania kwa kuwa wenyeji wa
fainali za Dunia ambapo mwaka 2006 fainali za dunia za Miss Touris World
2006 zilifanyika nchini na kushirikisha nchi zaidi ya 100. Na Mwaka 2005
Tanzania iliingia katika historia ya Dunia ya Tasnia ya urembo kwa kutwaa taji
la kwanza la dunia kupitia kwa Miss Utalii Tanzania 2005 -Witness Manwingi,
huo ulikuwa ni mwanzo wa mfululizo wa mataji ya kimataifa
kila mwaka ambao Miss Utalii Tanzania walishiriki,ikiweo Miss Utalii Tanzania
kutwaa mataji ya dunia mwaka 2006 kupitia kwa Miss Utalii Tanzania
2006 -Killi Janga huko China Taipei, 2007 kupitia kwa Miss Utalii
Tanzania 2007 - Lilian Siprian huko Uturuki n.k.
Tangu Kusitishwa kwa mashindano
ya Miss Utalii
Tanzania nchini mwaka 2013, tasnia ya urembo nchini imedorola kabisa na
kupoteza msisimko uliokuwepo kabla ya kusitishwa kwa mashindano hayo.
Ni matarajio
yetu kwamba ujio mpya wa mashindano Miss Utalii Tanzania, baada
ya kukamilisha taratibu zote za BASATA itakuwa ni chachu ya
kurudisha msisimko na hadhi ya mashindano ya urembo na mitindo
nchini.
Bodi ya
Miss Utalii Tanzania
imesikitishwa sana
na hali ya kudorola kwa sanaa na tasinia ya urembo na mitindo
nchini.
Asante,
Gideon E.
Chipungahelo
Mkiti Mtendaji Bodi
ya Miss Tourism Tanzania
Organisation
No comments:
Post a Comment