BASATA YAIDHINISHA
MABADILIKO MAKUBWA NA KIHISTORIA
YA MASHINDANO YA MISS UTALII
TANZANIA
Baraza la Sanaa la Taifa
(BASTA),limeidhinisha mabadiliko yaliyo fanywa na bodi ya mashindano ya shindano
la Miss Utalii Tanzania, mabadiliko hayo tunayoweza kuyaita ya kihistoria na
mageuzi makubwa ya sanaa ya urembo nchini, yameidhinishwa sambamba na Baraza la
sanaa kuruhusu kuanza kufanyika tena kwa mashindano haya ya pekee nchini,ambayo
mbali ya bodi ya mashindano kuyasitishakwa muda , BASATA iliyafungia kwa muda
usio julikana,kwa masharti ya kuitaka bodi ya mashindano haya kufanya maboresho
ya kuimarisha mfumo wa mashindano na uongozi,baada ya fainali za mwaka 2013.
Kwa muda wa zaidi ya miaka
mitano bodi tumekuwa tukifanya utafiti wa kisayansi na kimantiki kitaifa na
kimataifa, utafiti ambao ulihusisha pia nchi mbalimbali zenye mafanikio makubwa
katika sanaa ya urembo duniani, na kushirikisha taasisi mbalimbali za kitaifa
na kimataifa ,zikiwemo za Africa Tourism Promotion Centre na World Beauty
Pageant Association, ili kupata mfumo bora na sahihi wa uongozi na mashindano
haya adhimu nchini. Katika utafiti wetu,tulibaini haja ya shindano hili
kuendeshwa kitaasisi badala ya kikundi cha mtu au watu, kupitia mpango mkakati
maalum tulio upa jina la “Miss Tourism Tanzania at an Institution Level “
tuliona haja ya kuwa na mfumo rasmi wa uongozi (Organisation Structure) na
mfumo rasmi wa shindano ( Pageant Structure).
Aidha katika utafiti wa
faida na umuhimu wa shindano hili kwa jamii na taifa,tulibaini kuwa taifa
linaweza kunufaika kupitia mashindano haya kwa kutangaza kimataifa
Utalii,Utamaduni,Wanya mapori, Mazingira, Huduma za Misitu,Uwekezaji na
kuhamasisha kitaifa Utalii wa ndani,Utalii wa Kitamaduni,Utalii wa
Michezo,Utalii wa Mazingira na Utalii wa Mikutano,Vita dhidi ya Uwindaji na
Uvuvi Haramu,Vita dhidi ya Uharibifu wa Mazingira na Misitu,vita dhidi ya
tamaduni kongwe na potofu,vita dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji wa
kijinsia,wanawake na watoto. Hivyo kufuatia utafiti huo bodi imechukua hatua ya
kuanzisha mfumo rasmi wa uongozi (Organisation Structure) na mfumo rasmi wa
shindano (Pageant Structure),ambao umetoa mgawanyo wa madaraka ,majukumu na
wajibu katika ngazi zote za mashindano,na kuwa na uwajibikaji wa pamoja wa
kitaasisi (responsibility accountabilities),hivyo kuanzia sasa Miss Utalii
Tanzania ni Taasisi ya rasmi ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania, iliyo
sajiliwa kwa mujibu wa sheria zote za usajili za kitaifa na kimataifa.
Aidhapia katika kukabiliana na changamoto ya kutimiza wajibu wa shindano hili kwa Taifa, bodi imelibadili na kuwa shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania (Miss Tourism Tanzania International Pageant) kuanzia sasa. Ambapo shindano litakuwa na washiriki wa kitaifa wanao wakilisha kanda maalum nane (8) za Tanzania na washiriki wa kimataifa wawakilishi wan chi mbalimbali Duniani. Kanda za ngazi ya kitaifa za mashindano haya ,zimegawanywa kuzingatia Nyanja za kiutawala naza kiutalii, kanda hizo ni Miss Utalii Kanda ya Kusini, Kaskazini, Mashariki, Magharibi, Kati, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini, na Pwani. Hatua ya kulifanya shindano kuwa la kimataifa na mgawanyo wakikanda,unalenga kutoa fulsa kwa Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia washiriki watakao kuja kutoka nchi mbalimbali duniani,tofauti na awali ambapo Tanzania ilikuwa ikitegemea kujitangaza kupitia washindi wetu kwenda katika nchi nyingine kushiriki mashindano yanayo andaliwa au kufanika huko,,kinyume na ukweli kuwa wanafalsafa wote wa matukio ya kimaadhimishao ya kimataifa duniani,wanakubaliana kuwa nchi hunufaika pale tukio la kimaadhimisho linapo fanyika katika nchi husika,na sio kupeleka washiriki kushiriki katika nchi nyingine,na kukumbushakuwa washiriki huwa ni mabango ya matangazo ya nchi wenyeji.
Ujio mpya wa shindano hili wa Miss Tourism at an International Level ni fulsa nyingine kwa Taifa na jamii kitalii,kiuchumi na kijamii,na kipekee kiwekezaji, fainali za Taifa za kimataifa zimepangwa kushirikisha washiriki 100 ,toka nchi 100 duniani,, na washiriki 40 kutoka mikoa ya kanda 8 za Tanzania, fainali hizo zitarushwa LIVE duniani kote na kushudiwa na zaidi ya watazamaji 922,000,000 duniani kote. Kalenda rasmi ya mashindano haya,ambayo sasa tumekuwa na kalenda ya kudumu ya mashindano ,itatangazwa katiak mkutano na semina ya kimataifa ya waandishi na vyombo vya habari itakayo fanyika hivi karibuni. Hata hivyo kalenda ya kudumu ya mashindano haya , imelifanya shindano hili kuwa sehemu ya maazimisho ya sherehe za Taifa za suhuru wa Tanzania kila mwaka,na kuileta Dunia kuwa sehemu ya sherehe za Uhuru wa Tanzania kila mwaka, huku wakitangaza Utalii,uwekezaji,huduma za misitu,wanyama pori na mazingira ya Tanzania duniani kote.
Malengo ya shindano hili pia yameborehwa ili kukidhi matakwa ya kuwa shindano la kimataifa, bila kuathili tamaduni na mila njema za Tanzania na Afrika. Malengo mahususi ya mashindano haya ni kuunga mkono juhudi zaserikali na mamlaka zake ,kwa kutafsiri kwa vitendo sera za Taifa za Utalii, Utamaduni, Michezo, Wanyama pori, Misitu, Uwekezaji, Mazingira, Biashara, Viwanda,wanawake , Jinsia na Watoto kitaifa na kimataifa.
Mashindano ya kimataifa ya Miss Utalii Tanzania (Miss Tourism Tanzania International Pageant ), ni tafsiri ya vitendo ya sera za Taifa za Utalii,Uwekezaji,Mazingira,Wanyamapori,Misitu,Mambo ya Nje na Maendeleo ya Jamii , lakini pia ni uungaji mkono kwa vitendo wa juhudi na hatua za serikali ya awamu ya tano ,chini ya uongozi madhubudi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mheshimiwa John Pombe Magufuli, ambapo tumeshudia sekta ya Utalii ikipewa uzito stahiki na kuchukua sura mpya kitaifa na kimataifa,. Nasi tunaamini wakati sasa umefika teana wakati sahihi kwa kila mmoja wetu kuunga mkono na kushiriki kwa namna moja au nyingine katika kukuza Utalii,ambao ni kati ya sekta muhimu katika uchumi wa taifa letu,ambapo sasa utana changia zaidi ya 25% ya pato la fedha za kigeni,na 17% ya pato la Taifa ,lakini sekta ya Utalii ina changia 12% ya ajira zote Duniani, ikiwa na maana kuwa katika kila ajira 100 ,basi 12 zimetokana na utalii.
No comments:
Post a Comment