Miss Tourism Tanzania Organisation & Africa Tourism Promotions Centre aiming at the promotion of Tourism, Culture, Wildlife, Environments, Forest Services, Investments, Other Natural Resources, Social and Economic Developments. We are an organizer of Miss Tourism Tanzania National and International, Miss Tourism University World, Miss Tourism University Africa & Miss Tourism Pageant Africa. We do Great safari Fashion Show
FAINALI ZA DUNIA ZA MASHINDANO YA UREMBO ZAKWAMISHWA NA KORONA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI/UMMA 18-11-2021
Yah: WIMBI JIPYA LA CORONA LAAHIRISHA FAINALI ZA DUNIA:MISS AFRICA GOLDEN 2021, MISS UNITED NATION 2021, MISS WISDOM WORLD 2021 NA MISS TOURISM WORLD 2021
Fainali za dunia za mashindano mbalimbali ya ulimbwende zimeahilishwa kufuatia tahadhari za wimbi jipya la UVIKO 19, (COVID 19) katika baadhi ya nchi duniani. Fainali hizo za zilizo aihirishwa, ambazo Tanzania inawakilishwa na warembo wa shindano la Miss Utalii Tanzania, ni pamoja na fainali za dunia za:
Miss Wisdom World 2021 , zilizo kuwa zifanyike nchini Vietinam kuanzia Novemba 16 hadi 26, 2021,SASA ZITAFANYIKA MWEZI Machi 2022 ambapo Tanzania ilikuwa inawakilishwa na Miss Utalii Tanzania 2020/2021 - Nasra Ally Mohamed, ambazo sasa zitafanyika mwakani 2022. Miss United Nation 2021, zilizo kuwa zifanyike nchini India kuanzia Disemba 1 hadi 7 ,2021, ambapo Tanzania inawakilishwa na Miss Utalii Tanzania 2021- Kanda ya Mashariki , Judith Ngusa, sasa zitafanyika mwakani nchini India kuanzia Februari 1 hadi 7,2021.
Miss Africa Golden 2021, zilizokuwa zifanyike nchini Uturuki kuanzia Novemba 20 hadi 29, 2021, sasa zitafanyika Dubai tarehehe 15 hadi 23 Januari 2022 ambapo Tanzania inawakilishwa na Miss Utalii Tanzani 2021 – Arusha , Sharon Ahimidiwe Mmari, sasa zitafanyika mwakani ,katika jiji la kitalii na kibiashara la Dubai.
Miss Heritage Globe 2021, sasa zitafanyika Tanzania 2022, Miss Tourism World ambayo mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2019 nchini Serbia, sasa itafanyika Tanzani mwakani 2022, baada ya kushindikana kufanyika Antalya Uturuki, Miss Gold International 2021, iliyo kuwa ifanyike Venezuela Disemba sasa itafanyika mwakani, Miss Environments International 2021,iliyo kuwa ifanyike india,sasa itafanyika mwakani, Miss Tourism Intercontinental 2021 , sasa itafanyika kwa njia ya mtandao nchini Malaysia , Miss Ecology International sasa itafanyika India 2022, Miss Eco Tourism World sasa itafanyika Tanzania 2022 na Miss Tourism University World, sasa itafanyika Tanzania 2022.
Akifafanua zaidi , juu ya kuahirishwa kwa mashindano hayo, Erasto Gideon Chipungahelo, Rais wa Miss Tourism Tanzania Organisation, ambaye pia ni mkurugenzi wa Taifa wa mashindano hayo yote, kumegawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza ni kwa nchi wenyeji kuwa na sheria ya watu wote wanao ingia wakae katika uangalizi kwa siku kumi na nne ikiwemo Uturuki ambako Fainali za dunia za Miss Africa Golden 2021 ilikuwa zifanyike na zile ambazo haziruhusu watu kuingia wala kutoka nchini mwao ikiwemo Vietnam ambako Fainali za dunia za Miss Wisdom 2021 ilikuwa zifanyike.
Iwapo hali itaendelea kuwa hivyo, kwa washiriki kushindwa kutoka katika nchi zao au kuingia katika nchi nyingine ,kuna kila dalili kuwa tasnia ya Urembo itachukua sura mpya kwa kufanyika mitandaoni “Online”
Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2021, zitafanyika mapema Disemba 2021, ambapo kambi ya Taifa ya Fainali hizo zitakazo shirikisha warembo 50 wenye mataji ya mikoa na kanda itaanza mwishoni wiki ya mwisho ya Novemba 2021, jijini Dar Es Salaam, Bagamoyo na Morogoro. Hizi zitakuwa ni Fainali za kwanza chini ya kanuni na taratibu mpya za shindano hili , zitakuwa ni Fainali za saba ,baada ya kutofanyika kwa miaka tisa baada ya Fainali za mwisho zilizo fanyika
Kuahirishwa kwa Fainali mbalimbali za dunia hakuta athiri nafasi za warembo walio pata nafasi za kuwakilisha nchi zao katika Fainali za 2021, kwani kwa mujibu wa sheria za kimataifa wao ndio watakao wakilisha nchi zao 2022, lakini pia haita athiri ushiriki wa washindi wa Taifa wa Miss Utalii Tanzania 2021, ambao wata wakilisTanzani katika Fainali za mashindano 10 ya dunia kulingana na vigezo vya kila mmoja miongoni mwa watakao ingia kumi bora ya taifa na kipaji.
Mkwakwani Tanga mwaka 2013 , na Hadija Saidi Miss Utalii Morogoro 2012 kuibuka mshindi wa Miss Utalii Tanzania 2013/2014, na kuwakilisha Tanzania katika Fainali za dunia za Miss Tourism World 2013, zilizo fanyika nchini Equatorial Guinea.
Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa
Asante,
Erasto Gideon
Rais Miss Tourism Tanzania Organisation
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment