Miss Tourism World 2005- Africa

Miss Tourism  World 2005- Africa
Africa Tourism Promotion Centre

NGORONGORO CRATER

NGORONGORO CRATER
We Welcome Miss University Tourism World 2014 Contestants to Africa

AFRICA TO HOST WORLD GREAT SAFARI TOUR 2014

AFRICA HONORED TO HOST 
WORLD GREAT SAFARI TOUR 2014
The Africa Tourism Promotion Centre (ATPC) ,International Event Organizing Board, have accorded Africa Continent to host ,"World Great Safari Tour" 2014, so as to sunspot Africa Continent Countries Efforts in Promotion and Protection of Tourism, Investments Opportunities, Environments and Wildlife Protection.
                       MISS UNIVERSITY TOURISM WORLD CONTESTANTS - National Costumes
Africa Tourism Promotion Centre, is an International Entity dedicated and committed at promotion and advertisements of  Tourism , Culture , Natural Resources , Investments Opportunities , Environments and Wildlife Protection at International and National Level , in the course of Hallmark International Events of Sports , Culture, Pageantry Tourism ,Tours and Carnivals ,Conferences,  Bonanza , Concerts etc                                               
  CONTESTANTS Crowning
We at Africa Tourism Promotion Centre we believes that Tourism Industry is a Powerful Poverty Elevation Tool and among major World's  Economic and Development contributor. However ,the Tourism Industry Growth mainly in Africa Countries face number of barrier few to mention are : Poaching, Weak infrastructures, High Promotion and Advertisement Cost, deficient in Domestic Tourism, Environment Distractions and lack of Tourism awareness among the Community and the Public, also break open between Tourism, Wildlife, and Environment Protections.
                                                                    CONTESTANTS Beach Wear
We believe ,The Time is Now  ,the right Time for Public and Private Sectors  to Join up our Hands and Efforts for Overcoming all The Tourism Growth and Development Barriers so that we promote Tourism ,Culture, Environments,Wildlife, Tourism Investment Opportunities and Ant Poaching .That is why we have created "World Great Safari Tour" an international Event with capacity of Promoting Tourism,Tourism Investment Opportunities,Wildlife and Environment Protections (Ant Poaching) and stimulation of Tourism and Environments and Wildlife Protection awareness among the Public both at National (Host Country) and International Level.
                                                      CONTESTANTS - Evening Gown
World Great Safari Tour 2014, is a heavily Media Lead Events ,to be Televised and Streamed LIVE from Africa accorded Host Country to Worldwide,promoting and showcasing at large Host Country Tourism and Culture,Investment and Trade Opportunities,Goods and Services and mainly Ant Poaching, Environments and Wildlife Protection Efforts.
                                                              ANT POACHING
World Great Safari Tour 2014,will comprise Miss University Tourism World 2014 ,World Final ( With 120 Contestants ,120 Countries), Ant Poaching International Marathon 2014 , National Parks International Marathon 2014,Wildlife International Marathon 2014 all with More Than 100 Countries ,12,000 International and Local Athletics. Also comprises World Tourism Award 2014 in more than 21 Tourism Categories  , 
                                                   WORLD  GREAT SAFARI
and Great Safari Tour 2014 to Host Country Tourist Attractions (National Parks, Cultural Monuments,Historic Sites,Conservation Areas, Marine Parks) and of course in Street for Filming and Photo Shootings ( With More Than 480 International Participants  including Contestants and International Media Personnel), last but not the list World Great Safari Tour 2014 will also Comprise International Conference on Linking Tourism Growth, Environments and Wildlife Protection Agenda.
                                               ENVIRONMENT PROTECTION
Registration of  Delegates for Participation in The International Marathons,Tour,International Tourism Conference and Contesting for Miss University Tourism World 2014 is going on Direct International Organizing Board and National Directors worldwide.
Dates and Host Country to Be Announced shortly

WORLD GREAT SAFARI OFFICIAL LOGO

MISS UTALII TANZANIA 2013, KUTANGAZA KITAIFA NA KIMATAIFA NYATI NA MAAJABU YA HIFADHI YA NGORONGORONYATI WA AJABU APATIKANA NGORONGORO -TANZANIA.
 
Miss tourism Tanzania contestant on action
Hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro Crater) ,imedhihirisha kuwa ni moja ya maajabu saba ya Dunia Afrika, kwa hivi karibuni kupatikana Nyati mwenye rangi nyeupe. Huyu ni Nyati wa pekee Tanzania na pengine Duniani kuwa na rangi hiyo,tofauti na Nyati wengine ambao rangia yao ya kawaida ni nyeusi. Bado wataalam wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wanafanya utafiti wa chanzo na asili ya nyati huyo mweupe,ambaye amekuwa kivutio hata kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo. Nae Miss Utalii Tanzania 2013,Hadija Mswaga ,amefurahishwa na tukio hilo ,ambalo amesema limeongezea idadi ya maajabu ya Ngorongoro Crater ,ambapo sasa yanafkia manne ikiwemo mchanga unao hama kwa kila mita 17 kila mwaka,unyayo na vuvu la binadamu wa kale zaidi Duniani, Binadamu na wanyama hayawani kuishi pamoja bila kudhuriana lakini pia uwepo wa wanyama katika bonde la Ngorongoro ambalo liko chini ya usawa wa bahari kwa zadi ya mita 210. Akiwa ni balozi wa Hifadhi ya Ngorongoro,ambao ndio wadhamini wakuu wa safari yake ya kwenda kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss Tourism World 2013, Hadija ameahidi kwenda kuitangaza Ngorongoro na maajabu yake,ili kuongeza idadi ya watalii na pato litokanalo na utalii katika hifadhi hiyo.

NYATI WA AJABU NGORONGORO                         


THE MISS TOURISM TANZANIA 2013
        
1ND RUNNER UP MISS TOURISM TANZANIA 2013
3rd Runner Up Miss Tourism Tanzania 2013

MISS UTALII/TOURISM TANZANIA 2013, KWENDA EQUATORIALGUINEA WIKI IJAYO
MISS UTALII TANZANIA KWENDA  
MISS TOURISM WORLD 2013
Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Mswaga, anaondoka nchini  kuelekea Equatorial Guinea kuwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Dunia ya Miss Tourism World 2013. Atasafiri kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airline.

MISS TOURISM TANZANIA 2013
 Katika mshindano hayo yanayo shirikisha nchi 126 duniani kote, na kuonyeshwa LIVE katika Televisheni Duniani kote, Miss Utalii Tanzania 2013, anabeba ujumbe wa kutangaza Hifadhi ya Ngorongoro Crater kama moja ya maajabu ya Dunia Afrika. Akitoa sababu za kuibiba Hifadhi ya ngorongoro katika mashindano hayo, Hadija Mswaga, alisema kuwa mbali ya hifadhi hiyo kuwa ni ya kipekee duniani, lakini ndiyo hifadhi ambayo chimbuko la binadamu wa kwanza kuishi duniani, pia hifadhi hiyo ndio kitovu cha hifadhi ya faru nchini, mbali ya kuwa ndiyo hifadhi pekee duniani ambako binadamu na wanyama wanaishi na kushirikiana maisha ya kila siku bila ya kudhuriana. Wakati sasa umefika tena wakati sahihi kwa hifadhi ya ngorongoro kuwa hifadhi kiongozi kwa umaarufu ,pato la utalii na kutembelewa na watalii wengi zaidi duniani alisema hadija.
TOP 5 MISS TOURISM TANZANIA 2013.WITH KOKORIKO DESIGNER

WASHINDI WA DUNIA MISS UTALII TANZANIA

MISS UTALII TANZANIA WASHINDA MATAJI YA DUNIA


 MISS TOURISM WORLD 2005- AFRICA- Witness Manwingi

 Miss Tourism World 2005- Africa Witness Manwingi 

             Miss Tourism World 2005- Africa                                     Witness Manwingi
Miss Tourism World 2005- Africa                Witness Manwingi
Miss Tourism World 2005- Africa 
Witness Manwingi
Miss Tourism World 2003 - Irina Selugariou and  
Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi
 Miss Tourism World 2005- Africa 
Witness Manwingi
Miss Tourism World 2006 – SADC 
Killy Janga Left
 Miss Tourism World 2007 – Africa 
 Lillian Cyprian

Miss Tourism World 2008- Internet
Lilly Kavishe 1ST Left

TOP 5 MISS TOURISM TANZANIA 2013
MISS TOURISM TANZANIA 2013

BODI MISS UTALII TANZANIA YASIMAMISHA MASHINDANO KWA MWAKA MMOJA

THE MISS TOURISM TANZANIA 2013
BODI MISS UTALII TANZANIA YAFANYA MAAMUZI MAGUMU.
Yasimamisha shindano kwa mwaka mmoja
Bodi ya taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), yenye dhima ya kikomo ya kuratibu na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imetangaza kusimamisha kufanyika  mashindano hayo katika ngazi zote kwa msimu wa 2013/2014. Lengo la kutofanya mashindano hayo kwa mwaka mmoja  ni kujipanga upya na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa mashindano katika ngazi zote.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT SAADANI NATIONAL PARK

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo Erasto Gideon Chipungahelo, uamuzi huo mgumu umechukuliwa na bodi ya mashindano hayo wakati wa kikao cha tathimini ya miaka mitano ya mashindano hayo, na miaka kumi ya taasisi ya Miss Tourism Tanzania Organisation ambayo ilisajiliwa na kuanzishwa rasmi mwaka 2002,sambamba na usajili wa mashindano hayo. Fainali za kwanza za Miss Utalii Tanzania, zilifanyika mwaka 2004katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam, na fainali za tano za Miss Utalii Tanzania zilifanyika Mei 19,2013 katika uwanja wa mkwakwani Tanga.
 
MISS TOURISM TANZANI 2013 AT SAADANI N/ PARK
Bodi katika tathimini hiyo ya ndani imebaini changamoto mbalimbali za kimfumo,udhamini, utendaji,kuporomoka au kudumaa kwa sanaa ya urembo nchini na hujuma. Mfumo DUME wa uendeshaji wa mashindano ya urembo nchini kikwazo kwa ukuaji wa wazo au ubunifu wa kazi ya sanaa husika, kwani bodi imebaini mfumo  huo kutoa mianya ya hujuma na kupindishwa kwa wazo na lengo mama la mbunifu.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT WAMI RIVER SAADANI NATIONAL PARK

Lakini pia mfumo DUME wa udhamini, umekuwa ni kikwazo na changamoto kubwa kwa ukuaji wa sanaa nchini, kwani mfumo uliopo wa udhamini unatoa fulsa ya wadhamini kuwa wafalme au miungu watu , kiasi cha kudhamini kisicho bora,kisicho na mafanikio, kisicho na tija katika jamii na kuacha kudhamini kilicho bora,chenye tija katika jamii na kilicho na mafanikio makubwa kitaifa na kimataifa. Kwa visingizio na sababu mbalimbali mfumo wa udhamini nchini umekuwa ukitoa fulsa kwa wadhamini kuwa waandaaji na kupotosha kabisa maudhui ya ubunifu wa sanaa husika. Mfumo wa udhamini nchini umezaa aina mpya ya Utumwa wa kujitumikisha na kuwafanya wabunifu wa kazi za sanaa kuwa watwana na wadhamini kuwa mabwana mkubwa.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT SAADANI NATIONAL PARK

Kwa zaidi ya miaka 18 sasa tangu kuanza upya kwa sanaa ya urembo nchi, tumeshudia kuanzishwa na kufa au kuuawa kwa mashindano na kazi mbalimbali za ubuni fu wa sanaa hii. Aidha katika kipindi hiki tumeshudia kuporomoka kwa kasi ya ajabu kwa sanaa ya urembo nchini,tofauti na nchi jirani na nyinginezo duniani. Kuporomoka ambako kumepelekea umaarufu wa matamasha ya urembo nchini kuporomoka. Zipo sababu nyingi za kuporomoka kwa sanaa hii nchini, chache kati ya hizo ni Mfumo DUME wa Udhamini, kutotambua unyeti wa taaluma ya sanaa ya urembo kuwa ni wazo na ubunifu wa mtu kwa msukumo nafsi wa mtizamo,fikra na imani ya kuamini katika ndoto yake. Hii inamaana kuwa tofauti na michezo au sanaa nyingine sanaa ya urembo hususani mashindano ya urembo hayana fomila wala mfumo yakini, kama ilivyo kwa mpira wa miguu,au muziki au uigizaji wa filamu, uchezaji na upigaji wa ngoma za asili n.k, hivyo kwa kiasi kikubwa hutegemea ubunifu na mtizamo wa mbunifu wa shindano husika katika kufikia ndoto ya ubunifu na matarajio yakea juu ya wazo husika.
MISS TOURISM TANZANIA 2013, AT SAADANI NATIONAL PARK

Bodi imebaini kuwa mifumo ya uendeshaji iliyopo inatoa mianya ya hujuma baina ya shindano na shindano na hata baina ya wadhamini wa shindano flani na jingingine, lakini pia baina ya wabubunifu na mafisadi wa kazi za sanaa za wabunifu wajasilia mali.Hapa hujuma zimegawanyika katika makundi tofautitofauti ikiwemo waraembo mamluki wanao pandikizwa katika mashindano mengine, viongozi au wajumbe wa kamati mamluki na wale wenye uchu wa madaraka na kuvuna bila ya kupanda, lakini hujuma kupitia propaganda chafu, fitina,majungu na kupakana matope. Zipo hujuma pia za watu wa kada mbalimbali katika jamii kutumiwa kufanikisha adhma ya mafisadi wa kazi za ubunifu wa sanaa na upindishaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo duniani na sanaa nzima ya urembo kitaifa na kimataifa.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT  DAR ES SALAAM UNIVERSITY  (SJM) 
Udhamini na hujuma imekuwa ni changamoto kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania. Tofauti na mtizamo wa wengi kuwa tumekuwa tukipata udhamini na wadhamini wakubwa katika Miss Utalii Tanzania , ukweli ni kwamba hakuna udhamini wowote mkuu na mkubwa tunao upata kutoka kwa sekta binafsi wala ya umma, badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali zetu na nguvu zetu kufanikisha kufanyika kwa fainali za kila mwaka , ikiwemo kugharamia ushiriki wa washindi wa Taifa katika mashindano ya Dunia , japo katika mashindano yote 6 ya Dunia na mengineyo ya kimataifa tume peperusha vyema bendera ya Taifa  na Utalii wa Tanzania kwa kutwaa mataji katika mashindano yote tuliyo shiriki, tunashikilia zaidi ya mataji 7 ya Dunia hadi sasa.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 CONTESTANTS
Mafanikio haya ya kimataifa matunda yake ni pamoja na Tanzania kupewa heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za Dunia za Miss Tourism World 2006. Fainali ambazo kwetu zimekuwa kama mwiba wa mchongoma kutokana na watu wengi kudhani kuwa udhamini tulio upata wa serikali ulikuja kwetu, wakati ukweli ni kwamba fedha zili zilikwenda Miss Tourism World Organisation na kulipa watoa huduma wa ndani walio hudumia huduma mbalimbali zikiwemo za malazi, chakula, usafiri, matangazo, ulinzi, kumbi, taa na majukwaa.
 
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT MIKUMI NATIONAL PARK
Ni kama mwiba wa mchongoma kwetu kwa sababu, wengi wanadhani na kuamini kuwa Miss Utalii Tanzania, tunapata udhamini wa mamlaka za utalii, wakati ukweli ni kwamba hakuna udhamini kama huo. Licha ya ukweli kuwa katika umri wake wa miaka Miss Utalii Tanzania ndilo shindano lenye mafanikio makubwa zaidi kitaifa na kimataifa kuliko mashindano mengine yoyote nchini na hata Afrika mashariki na kati. Udhamini ni changamoto na kikwazo kikuu cha kufikia 100% ya malengo ya shindano letu na hata ndoto yetu ya kulifanya kuwa shindano bora zaidi nchini,Afrika na hata Duniani. Baadhi ya mataji ya Dunia tunayo shikilia ni pamoja na Miss Tourism World 20050 - Africa, Tourism Model Of The World 2006- Personality, Miss Tourism World 2006- SADC, Miss Africa 2006 – 1st Runner Up, Miss Tourism World 2007- Africa, Miss Freedom Of The World 2013, Miss Tourism World 2008 -Internet, Miss United Nation 2009.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT MIKUMI NATIONAL PARK
Miss Utalii Tanzania ni shindano la kwanza nchini kutwaa taji la Dunia kabla na baada ya uhuru na kuipa Tanzania heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za Dunia 2006. Rais wa Miss Tourism Tanzania Organisation Gideon Chipungahelo, ni mtanzania wa kwanza kuteuliwa katika uongozi wa ngazi ya Dunia wa Urembo, ikiwemo nyadhifa za Mkurugenzi Bara la Afrika Miss Tourism World Organisation, Miss United Nation Organisation na Makamu wa Rais Dunia World Beauty Pageant Association, Miss Tourism University World Organisation na Miss Heritage World Organisation. Ili kukabiliana na changamoto hizi, bodi ya mashindano imebadili sera na mfumo wa uongozi na uendeshaji mashindano, kutoka katika mfumo wa kuwa shindano la kibiashara hadi kuwa shindano la kijamii (Non Profit Making), kutoka katika mfumo wa kufanya shindano stejini kuanzia ngazi za chini hadi katika mfumo wa kufanya mashindano stejini kuanzaia katika ngazi za kanda na klanda maalum za vyuo vikuu, kutoka katika mfumo wa kuwa na kamati na mawakala hadi katika mfumo wa kuwa na wakurugenzi waajiliwa wa ngazi za kanda hadi taifa, na kuwa na kamati zenye majina makubwa hadi kamati za wataalam watendaji. 
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT MIKUMI NATIONAL PARK
Kutoka katika mfumo wa onyesho la viingilio hadi katika mfumo wa onyesho lisilo na viingilio, kutoka katika mfumo wa onyesho la ukumbini hadi katika mfumo wa onyesho la TV Show. Kutoka katika mfumo wa kuweka kambi katika mahoteli hadi katika mfumo wa kuweka kambi katika Miss Tourism Houses na Tourist Attractions Camp Sites, kutoka katika mfumo wa kuwa shindano la kitaifa hadi katika mfumo wa kuwa shindano la kimataifa, lenye washiriki kutoka mabara yote duniani.
 
MISS TOURISM TANZANIA 2007
Kwa mfumo huu mpya, washindi wa ngazi za majimbo,wilaya na mikoa watapatikana kwa njia ya Odiashion. Kwa mfumo huu mpya kila mbunge atakuwa na mrembo wake wa Utalii, Kila Mkuu wa Wilaya atakuwa na Mrembo wake wa Utalii na Kila Mkuu wa Mkoa atakuwa na Mrembo wake wa Utalii. Lakini pia mfumo huu utadhibiti hujuma na ,umamluki, udanganyifu wa sifa za washiriki lakini pia kuondoa tatizo la warembo wasio na sifa , wasio natabia njema na mwenendo mwema katika jamii. Kwa mfumo huu wa TV Show, fainali zote kuanzia ngazi ya kanda zitarushwa LIVE katika TV na mitandao ya Internet. Aidha kwa mfumo huu tutakuwa na kituo chetu cha Televisheni cha Miss Tourism (Miss UTalii TV).
MISS TOURISM TANZANIA 2013
 Mkakati huu, ni mkubwa na unahitaji muda na umakini wa hali ya juu, pia wataalam wa ndani na nje kuufanikisha . Hivyo bodi imeona ni vyema kujipa muda wa mwaka (Msimu) mmoja kujipanga bila ya kufanya mashindano. Hapa ieleweke kuwa hatuja simamisha shughuli za kampuni za kutangaza na kuhamasisha utalii na utamaduni, bali tumesimamisha shindano la msimu wa 2013/2014, huku washindi wa msimu wa 2012/2013 wakiendelea na majukumu yao kama kawaida , ikiwemo kuwakilisha Taifa katika mashindano ya Dunia na kimataifa 2013/2014 kama ifuatavyo na nchi yanakofanyika katika mabano ni,
THE MISS TOURISM TANZANIA 2013
 Miss Tourism World 2013 ( Equatorial Guinea), Miss Face Of The World 2013 ( Afrika Kusini) , Miss Heritage World 2013 (China) Miss Tourism United Nation 2013 ( Marekani), Miss International 2013 ( Japani), Miss Planet 2013 ( Ufaransa ), Miss Tourism University World 2013 (Uingereza).
MISS TOURISM TANZANIA 2013
Aidha bodi imetoa onyo kali kwa yeyote atakaye thubutu au kujaribu tena kuhujumu shiondano hili kwa namna yoyote, kwani atakumbana na hatua kali za kisheria bila ya kujali wadhifa, mamlaka, jinsia au rangi. Bodi pia imewataka maadui na mamluki wote kujiondoa katika shindano hili na ngazi mbalimbali za uongozi na mataji kabla ya kuondolewa, kwani mchakato ujao hautalengwa kwa jiwe.
Erasto Gideon Chipungahelo
Mwenyekiti Mtendaji
Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO)