MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL

MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL
Miss Tourism Tanzania Pageants

Miss Tourism Tanzania Pageant

Miss Tourism Tanzania Pageant
We Welcome Miss Tourism Tanzania Organisation

Miss Tourism World 2005- Africa

MISS TOURISM TANZANIA PAGEANT

AKUDO IMPACT - WAZEE WA MASAUTI KUTUMBUIZA SHINDANO LA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 – VIPAJI


AKUDO IMPACT - WAZEE WA MASAUTI KUTUMBUIZA SHINDANO LA TAIFA
MISS UTALII TANZANIA 2012/13 – VIPAJI
Bendi ya Akudo Impact wazee wa masauti ,siku ya Jumapili tarehe 17, Februari 2013, itatoa burudani katika shindano la Taifa la kumsaka Mrembo wa Utalii mwenye kipaji kati ya warembo 40 waliopo kambini Ikondelelo Lodge wakijiandaa kushiriki Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 zitakazo fanyika mwisho wa mwezi huu katika Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.
Katika shindano hilo la Vipaji , ambalo litafanyika katika Ukimbi wa Jeshi wa Msasani Beach Club Jumapili kuanzia saa nane mchana ,pamoja na Bendi hiyo ya Akudo Impact , wasanii wengine watakao tumbuiza ni pamoja na mwanamuziki wa kimataifa Che Mundugwao, Msanii mdogo chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Geneous na burudani za ngoma za asili kutoka katika kundi kongwe la Kaole  Sanaa Group wakiomgozwa na mwana dada mahili katika uchezaji wa ngoma za asili Mariam Kweji aka kalunde wa Bongo Movie.
Shindano hilo la Vipaji ni moja ya mashindano ya awali ya kuwania tuzo mbalimbali kabla ya Fainali kuu,ambapo washiriki wote watashindana kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za makabila mbalimbali ya mikoa wanayo iwakilisha. Mikoa hiyo na majina ya washiriki katika mabano ni  Arusha (Rose Godwin), Dar es Salaam 1 (Sophia Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas),Dodoma (Erica Ekibariki), Geita (Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob), Kagera 1(Elline Bwire),  Kagera2 (Jania Abdul), Kagera 3(Mulky Uda),  Kilimanjaro (Anna Pogaly), Lindi (Joan John), Mtwara (Halima Hamis),Mara (Dorine Bukoni), Manyara (Mary C. Lita), Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro (Hadija Said),Tanga (Sarafina Jackson), Ruvuma 2 (Leah Makange), Tabora (Magreth Malalle), Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi (Asha Ramadhani ), Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma (Furaha Kinyunyu), Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel), Pwani (Beatrice Iddy), Singida (Neema Julius), Singida (Christina Daud),Vyuo Vikuu (Irine Richard), Vyuo Vikuu (Hawa Nyange)
Wakizungumzia kwa nyakati tofauti shindano hilo la Vipaji,Rais wa Miss Tourism Tanzania International Organisation ,wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo , alisema kuwa mandalizi karibu yote yamekamilika kuanzia ngazi za warembo hadi burudani za bendi, ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya. Hili litakuwa ni tukio kubwa na la kihistoria kuwahi kufanyika Tanzania ambapo Utalii, Urembo na Utamaduni wa ngoma za asili vitaonyeshwa kwa pamoja jukwaani, lakini kivutio cha pekee ni jinsi mabinti wa kizazi kipya tena warembo kutoka mikoa yote ya Tanzania na vyuo Vikuu watakavyo onyesha maajabu ya kusakata ngoma za asili kwa umahili mkubwa na wa pekee.
Shindano la Miss Utalii Tanzania mwaka huu limedhaminiwa na wadhamini mbalimbali wakiwemo Coca Cola Kwanza Limited, Daja Salon, Mtwana Catering Services Enterprises, Zizzu Fashion, Global Publishers, Ikondelelo Lodge, Clouds Media Group, Tone Media Group,Valley Spring na www.misstourismorganisation.blogspot.com
Katika Shindano hili viingilio vitakuwa ni kama ifuatavyo 5,000 kwa viti vya kawaida, 10,000 kwa V.I.P 2, na 30,000 kwa V.I.P 1 pamoja na Chakula.
Asante,
Erasto G. Chipungahelo
Rais


No comments: