MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL

MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL
Miss Tourism Tanzania Pageants

Miss Tourism Tanzania Pageant

Miss Tourism Tanzania Pageant
We Welcome Miss Tourism Tanzania Organisation

Miss Tourism World 2005- Africa

MISS TOURISM TANZANIA PAGEANT

SERIKALI YAWAPIGA MSASA WASHIRIKI WA FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13











Serikali yawapiga Msasa Washiriki  Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania  2012/13

Serikali kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii,imeendesha semina ya washiriki wa Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania 2012/13 iliyo fanyika leo Katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao makuu ya Bodi ya utalii Tanzania.

Semina hiyo ambayo ilifunguliwa na Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo Ndugu Devotha Mdachi, imeandaliwa na Bodi ya Utalii kwa lengo la Kuwapiga msasa washiriki hao kabla ya fainali ya Taifa itakayo fanyika 17.03.2013 katika ukumbi wa Dar Live.

Akifungua Semina hiyo Ndugu Devotha mdachi pamoja na kuwakaribisha washiriki wote makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania aliwaasa washiriki hao kujifunza na kuvielewa kwa kina vivutio vya utalii Tanzania ili wale watakao shinda na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia waweze kuitangaza vema Utalii wa Tanzania na nchi kwa Ujumla. Aliwakumbusha pia wao kama warembo wa utalii wanalo jukumu la kuunda mkono juhudi za Serikali kuhamasisha utalii wa Ndani lakini pia jukumu la kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa na Kimataifa. Aliendelea kuwaasa pia wao kama warembo wa utalii wanapaswa kujivunia utanzania na Maliasili zake huku wakidumisha Mila na Utamaduni wa Tanzania na kwamba siku zote wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu na mfano wa kuigwa katika jamii kwa maana warembo wa utalii ni alama ya Urithi wa Taifa na kielelezo cha Mwanamke wa Kitanzania. Aliwakumbusha wale watakao shinda kwenda kutetea Mataji ya Dunia ambayo Miss Utalii Tanzania wanashikiria .

Nae mtoa mada Mkuu katika semina hiyo Ndugu Deogratias Malogo ambaye ni Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa Bodi ya Utalii Tanzania aliwafahimisha warembo wa Miss Utalii Tanzania wa Fainali za Taifa 2012/13 kuwa secta ya utalii ni secta muhimu katika Uchumi na kuchangia pato la Taifa kila mwaka. Alisema Secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 20 ya pato la tTaifa kila mwaka na zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa la fedha za kigeni kila Mwaka. Alisema Kidunia secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 12 ya ajira zote Duniani.

Warembo hao walifundishwa Historia ya utalii Tanzania . Walifundishwa vivutio vya utalii Tanzania, Mbinu za kutangaza utalii wa Tanzania Kitaifa na Kimataifa, lakini aliwaelezea pia jitihada ambazo serikali kupitia bodi ya taifa ya utalii na Mamlaka nyengine za utalii nchini imekuwa ikifanya katika kukuza secta ya utalii na kutangaza vivutio vya utalii kitaifa na Kimataifa. Ndugu Malogo aliwaelezea juu ya umuhimu wa utalii wa ndani katika kukuza na kuchangia pato la utalii la Taifa na kwamba wao kama warembo wa utalii ni sehemu muhimu katika kukuza na kuendeleza secta ya Utalii Tanzania kwani wao ni kioo cha jamii na mfano wa kuigwa kitabia Mwenendo Muonekano na Hulka. Aliwatakia kila laheri wale watakao shinda katika fainali hizo za Taifa kwenda kuwa mabarozi bora wa Tanzania katika mashindano ya Dunia watakayo kwenda Kushiriki.

Nae Rais wa Miss Utalii Tanzania alitoa shukurani na Pongezi kwa Bodi ya Utalii Tanzania kwa juhudi kubwa wanazo fanya ya kuinua na kuendeleza secta ya utalii nchini. Alipongeza na kushukuru pia hatua ya bodi ya utalii, kwa kuendesha Semina Maalum kwa washiriki wa fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 na kusema kwamba semina hii itakuwa ni Dira na ufunguo kwa Miss Utalii Tanzania wa kutwaa mataji zaidi ya Dunia katika mashindano yote watakayo shiriki na pia katika kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani Kitaifa na Kimataifa.

Asanteni
Fredy Tony Njeje
Marketing and Public Relation Miss Utalii Tanzania.






No comments: