MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL

MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL
Miss Tourism Tanzania Pageants

Miss Tourism Tanzania Pageant

Miss Tourism Tanzania Pageant
We Welcome Miss Tourism Tanzania Organisation

Miss Tourism World 2005- Africa

MISS TOURISM TANZANIA PAGEANT

SIKU TATU KABLA YA FAINALI MAALUM YA SHINDANO LA VIPAJI DAR LIVE , BODI YA UTALII TANZANIA KUWANOA WASHIRIKI FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13.








Wakati maandalizi ya Fainali za Taifa za kumpata Miss Utalii Tanzania 2012/13 yakiwa yanaendelea kwa kasi kubwa, Bodi ya  Utalii Tanzania itaendesha Semina Maalum ya Mafunzo ya Utalii kwa washiriki wote walioko kambini Ikondolo Lodge Kibamba wakijiandaa na Fainali za Taifa zitakazo fanyika Mwishoni mwa wiki ijayo Jijini Dae es salaam.
Akithibitisha taarifa hizo  kwa  waandishi wa Habari Raisi wa  Kamati ya Mashindano hayo Erasto G. Chipungahelo  alisema kuwa Semina hiyo maalum itakayo endeshwa na Bodi yaUtalii Tanzania itafanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Utalii uliyopo katika ofisi za Bodi ya Utalii jingo la IPS Dar es salaamsiku ya Alhamisi Tarehe 7.03.2013 kuanzia saa Tatu asubuhi na kuwashirikisha zaidi ya Warembo 40 wakiwakirisha Mikoa yote ya Tanzania Bara , Kanda maalum za Vyuo vikuu na Zanzibar.  Watoa mada wakuu katika semina hiyo, itakuwa ni wataalam walio bobea katika secta ya utalii na masoko ya utalii kutoka Bodi ya Taifa ya Utalii(Tanzania Tourist Board).

Kwa niaba na kamati ya Miss Utalii Tanzania, Ninatoa shukurani za pekee kwa Serikali na Bodi nzima ya Utalii kwa kuendesha semina hii muhimu kwa washiriki wa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania ambapo washindi wa kwanza mpaka wa Tano watawakirisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya utalii ya Dunia. Yakiwemo ya Miss Tourism World, International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation World , Miss Tourism university World na Miss Heritage World. Yatakayo fanyika katika nchi mbalimbali kuanzia mwezi wa nne mwaka huu.

Hii ni fulsa ya pekee kwa washiriki na washindi watakao patikana katika fainali za Taifa kuweza kujua na kujifunza juu ya utalii Tanzania, mbinu na mikakati ya kutangaza vivutio vya kitalii kitaifa na kimataifa, hivyo kutusaidia kutimiza ndoto na malengo yetu ya miaka mitano ya kutwaa Mataji matatu ya Dunia mwaka 2013.

Maandalizi katika kambi ya warembo yanaendelea vizuri , ushindani ni mkubwa ari na dhamira ya kila Mrembo kulinda hadhi na Heshima ya Mkoa wake kwa kutwaa taji la Taifa ni kubwa.

Chipungahelo aliongeza kwamba, ili kuthibitisha hayo, anaomba watanzania wote wakazi wz Dar es salaam na Mikoa ya Jirani, wajitokeze kwa wingi siku ya ya Jumamosi Tar 9.03.2013 usiku katika ukumbi wa Dar Live Mbagala kushuhudia warembo hawa wakipanda jukwaani kuwania Tuzo mbalimbali za Vipaji na Utamaduni. Ambapo mbali na kupita jukwaani na mavazi mbalimbali washiriki wote pia watashindana kucheza na kuimba nyimbo za Asili za Mikoa wanayo wakilisha. Na hili litakuwa ni tukio la kihistoria la Utalii, Urembo na Utamaduni kuwahi kufanyika hapa Tanzania kabla na Baada ya Uhuru.

Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General Suppries Limited,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA ) www.misstourismorganisation.blogspot.com

No comments: