MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL

MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL
Miss Tourism Tanzania Pageants

Miss Tourism Tanzania Pageant

Miss Tourism Tanzania Pageant
We Welcome Miss Tourism Tanzania Organisation

Miss Tourism World 2005- Africa

MISS TOURISM TANZANIA PAGEANT

MISS UTALII DUNIA (MISS TOURISM WORLD 2013) KUFANYIKA EQUATORIAL GUINEA OKTOBA 12, 2013

FAINALI ZA DUNIA MISS UTALII (MISS TOURISM WORLD 2013)
 KUFANYIKA EQUATORIAL GUINEA OKTOBA 12, 2013
Fainali za Dunia za Miss Utalii 2013 (Miss Tourism World 2013),zitafanyika nchini Equatorial Guinea, trehe 2 ,Oktoba 2013. Fainali za Dunia mwaka huu zitashirikisha zaidi  ya nchi 100 kutoa dunia nzima ikiwemo Tanzania.
Katika fainali hizo za Dunia ambazo Tanzania itakuwa inashiriki kwa mara ya tano ,itawakilishwa na mshindi wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Saidi Juma (Pichani), ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2013. Hadija Saidi Juma, ambaye alitwaa taji la Taifa baada ya kuwashinda warembo wengine 29 kutoka mikoa yote ya Tanzania na Vyuo Vikuu katika fainali za Taifa , zilizo fanyika tarehe 9-5-2013 katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, ataondoka nchini tarehe 28-10-2013.

 Miss Utalii Tanzania imeijengea heshima kubwa Tanzania, sio kwa kuwa ya kwanza kutwaa taji la duni nchini tu,bali pia kwa kushinda mataji katika fainali zote za dunia tulizo shiriki, ambapo hadi sasa tunashikilia mataji manne ya Dunia. Mataji hayo na nchi yaliko fanyika katika mabano ni pamoja na Miss Tourism World 2005 –Africa (Zimbabwe), Miss Tourism World 2006 – SADEC (China Taipei), Miss Tourism Model Of The World 2006 – Personality (Tanzania), Miss Tourism World 2007 – Africa (Uturuki), Miss Africa 2006- 1st Runner Up na Miss Freedom Of The World 2013- Model. 

Maandalizi ya kumwandaa Miss Utalii Tanzania 2013, kwaajili ya kushinda taji la dunia,yanaendelea vizuri ,ili aweze kulinda heshima ya Tanzania na kuvuka rekodi ya warembo waliotangulia yanaendelea vizuri. Ambapo ili kuhakikisha ushiriki wake katika mashindano hayo ya dunia unakuwa na manufaa ya kutangaza Utalii wa Tanzania kimataifa, tumesha peleka maombi maalum Katika mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na mamlaka ya Hifadhi za Taifa ziweze kudhamini ushiriki huo na kufanikisha zaidi maandalizi.
 Tofauti na mashindano mengine, washiriki wote wa fainali hizo za dunia watapewa fulsa maalum ya kutangaza utalii na utamaduni wan chi zao kupetia vyombo mbalimbali vya habari duniani, jukwaani na nje ya jukwaa.Hii itkuwa ni fulsa nyingine ya pekee kwa Tanzania,TANAPA na Ngorongoro Crater kutangaza Hifadhi na vivutio vya utalii vya Tanzania kimataifa, kupitia Miss Utalii Tanzania 2013 katika mashindano hayo.

No comments: