Miss Tourism World 2005- Africa

Miss Tourism  World 2005- Africa
Africa Tourism Promotion Centre

NGORONGORO CRATER

NGORONGORO CRATER
We Welcome Miss University Tourism World 2014 Contestants to Africa

THE GIDEON

AFRIKA MASHARIKI WENYEJI “WORLD GREAT SAFARI TOUR” 2014/15.

MISS TOURISM CONTESTANT

Afrika ya Mashariki imepewa heshima ya kuwa wenyeji wa Tamasha la Dunia la Utalii,Michezo na Utamaduni (World Great Safari Tour 20114/15). Tamasha hilo ambalo litashirikisha zaidi ya nchi 120,litajumuisha Safari za kutembelea na kupiga picha za Video,Magazeti,Televisheni na Majarida ya kitaifa na kimataifa katika Vivutio vya Utalii,litajumuisha pia mashindano ya Dunia ya Mibio za Nyika ya kilomita 21 ya Ant Poaching International Marathon ,ya mita 10,000 ya National Parks International Marathon 2014/15 na ya mita 5,000 ya Wildlife International Marathon 2014/15, ambapo kwa upande wa utamaduni na burudani litajumuisha Ngoma za Asili na Mashindano ya urembo ya Dunia ya Miss Tourism University World 2014/15.Pia tamasha hili litajumuisha mashindano yam bio za magari na baisikeli ya Dunia.
 
MISS TOURISM
 Aidha Tamasha hilo litajumuisha Utoaji wa Duzo za Dunia za Utalii za “World Tourism awards 2014/15 na mashindano ya mchezo wa masubwi.
 
Tamashahilo litashirikisha washiriki wanamichezo,warembo,wasanii, wanamitindo wa kimataifa na watu mashuhuri na maarufu Duniani, wakiwemo wanadiplomasia na wana harakati wa kimataifa wa haki za Wanyamapori na mazingira kutoka nchi mbalimbali Duniani.Waandishi wa Vyombo vya habari vya kimataifa na kitaifa vya Televisheni ,Magazeti,Majarida ,Tovuti na Mitandao ya kijamii, watakuwa ni miongoni mwa washiriki wa Tamasha hilo,la kihistoria kuwahi kufanyika barani Afrika, hususani Afrika ya Mashariki. Likiwa linaandaliwa na Kampuni ya Africa Tourism Promotion Centre, Tamasha la World Great Safari Tour 2014/15, lita onyeshwa LIVE uniani kote kupitia Televisheni na Tovuti na Mitandandao ya Internet.
MISS TOURISM CONTESTANTS
 
Hii ni fulsa nyingine ya pekee kwa nchi ya Afrika ya Mashariki ,itakayo shinda Uteuzi wa kuwa wenyeji wakuu wa Tamasha hilo,kuonyesha duniani kote vivutio vyake vya utalii,mianya na fulsa za uwekezaji , lakini pia hii itakuwa ni fulsa kwa nchi hiyo kuonyesha Dunia juhudi za serikali yake,asasi binafsi na za umma katika kupambana na ujangili ,hususani uwindaji haramu,uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira,na kuvutia misaada na udhamini wa kitaifa na kimataifa katika kupambana na Ujangili,uharibifu wa mazingira na uwindaji haramu kwa ujumla.Nchi wenyeji itapata fulsa na heshima ya kuidhibitishia Dunia kuwa ni nchi yenye vivutio vya utalii,ni nchi yenye amani na salama kwa watalii na wawekezaji. Pia kuithibitishia Dunia kuwa ni nchi yenye uwezo na hadhi ya kuwa wenyeji wa matukio makubwa ya Dunia na mengine ya kimataifa, kimiundombinu, usalama, nguvu kazi na hata ukarimu na mahusiano ya kitaifa na kimataifa. 
 
MISS TOURISM
Mchakato wa kupata nchi wenyeji  wa Tamasha hili ,huanzia ngaziya kushindanisha mabara yote ya Dunia, ambapo bara la Afrika lilishinda, na hatua ya pili huwa ni kushindanisha kanda za bara husika ambapo Afrika ya Mashariki ilishinda. Hatua inayo fuatia sasa ni uteuzi wan chi ambayo itakuwa ndio wenyeji wakuu miongoni mwa nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki. Mazungumzu yapo katika hatua nzuri na serikali na baadhi ya asasi binafsi za nchi za Afrika ya Mashariki , na yatakapo kamilika tutaitangazia Dunia nchi iliyo shinda katika mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari,utakao fanyika katikla nchi hiyo husika.Katika uteuzi huo,tunazingatia vigezo mbalimbali, vikiwemo vya amani,ulinzi na usalama wa nchi husika, utayari wa nchi na serikali ya nchi husika wa kushirikiana kujitangaza kitaifa na kimataifa, uwepo na uhalisia wa vivutio vya kitalii katika nchi husika,uwepo wa juhudi na nia ya dhati ya nchi husika katika kupiga vita Ujangili,Uharibifu wa Mazingira na uwindaji haramu kwa ujumla. Na kubwa zaidi ni uwepo wa sera ya utalii ambayo inatambua kuwa utalii ni moja ya sekta madhubuti katika kukuza uchumi wa Taifa na kupiga vita umasikini.
MISS TOURISM
 
Hili ni tukio kubwa Duniani,ambalo litashirikisha washiriki zaidi ya 1500 kutoka zaidi ya nchi 120 duniani, wakitangaza utalii,utamaduni,michezo,huku wakipiga picha za video na Televesheni katika hifadhi za Taifa,Mapori ya akiba, na vivutio vingine vya utalii katika nchi wenyeji. Tukio hili kuu la kitalii Duniani litaonyeshwa LIVE duniani kote kupitia Televisheni na mitandao ya Internet , na kushudiwa na zaidi ya watazamaji Bilioni 1.5 duniani kote,huku waandishi wa habari wa kimataifa za Televisheni,Redio na Magazeti wakiambatana na washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani.
 
MISS TOURISM
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Makamu wa Rais Dunia – World Great Safari Tour/Africa Tourism Promotion Centre

No comments: