Miss Tourism World 2005- Africa

Miss Tourism  World 2005- Africa
Africa Tourism Promotion Centre

NGORONGORO CRATER

NGORONGORO CRATER
We Welcome Miss University Tourism World 2014 Contestants to Africa

THE GIDEON


ANCHI AFRICA MASHARIKI ZACHUANA UENYEJI TAMASHA LA UTALII LA DUNIA LA “WORLD GREAT SAFARI TOUR 2014/2015”
Miss Tourism Tanzania 2005
  Bodi ya Africa Tourism Promotion Centre, waandaaji wenye dhima ya kikomo ya kuratibu na kuendesha tamasha la Dunia la Utalii la “WORLD GREAT SAFARITOUR” 2014/2015 ,wakishirikiana na kampuni ya Miss Tourism Tanzania Beauty Pageant Limited, ipo mbioni kukamilisha mchakato wa kuteua nchi itakayo kuwa wenyeji wa tamasha hilo la kimataifa la Utalii.

Miss Tourism World 2005
 Katika hatua ya mwanzo mchakato huo ulishindanisha mabara yote ya dunia,yakiwemo  ya Asia,Ulaya,Marekani,Rusia, Asia,India na Afrika , ambapo bara la Afrika liliyabwaga mabara mengine na kuteuliwa kuwa wenyeji wa Tamasha hilo la Dunia. Katika hatua ya pili waandaaji walishindanisha kanda za bara la Afrika ,zikiwemo kanda za Afrika Magharibi,Afrika Kaskazini,Afrika ya Kati, na Kusini ambapo Afrika Mashariki iliibuka washindi na kupewa heshima ya kuwa  wenyeji wa Tamasha hilo la Dunia la World Great Safari Tour 2014/2015. 
 
                   Miss Tourism 2998
 Katika hatua ya mwisho ya mchakato wa kupata wenyeji wa tamasha hilo, nchi za kanda ya Afrika ya Mashariki zinashindanishwa ambapo nchi itakayo shinda kati ya Kenya,Burundi,Rwanda,Tanzania na Uganda ndiyo itakayo pewa heshima ya kuwa wenyeji wa Tamasha hilo kubwa la kimataifa la Utalii Duniani. 
 
Miss Tourism World 2005
Hii itakuwa ni fulsa ya pekee kwa nchi itakayo pewa heshima na hadhi hiyo kujitangaza kimatifa kiuchumi,kijamii na kubwa zaidi ni kutangaza Vivutio vyake vya Utalii,Mianya ya Uwekezaji na Fulsa ilizo nazo  za ushirikiano wa kimataifa, lakini pia utengamano wa amani na usalama kwa raia na wageni.
Miss Tourism 2005
 Aidha nchi itakayo shinda uenyeji huo, itapata fulsa ya kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili na Uharibifu wa Mazingira mkuithibitishia na kuionyesha jumuiya ya kimataifa na kitaifa Juhudi ambazo serikali ya nchi husika na mamlaka zake  inafanya katika kupiga vita Ujangili na Uharibifu wa Mazingira ,ikiwemo Uwindaji Haramu wa Misitu na Uharibifu wa Mzingira yakiwemo ya Hifadhi  Bahari na Nchi kavu.
Miss Tourism 2005

  Tamasha hilo ambalo litaonyeshwa moja kwa moja (LIVE) duniani kote kupitia Televisheni na Mitandao ya Internet , litajumuisha zaidi ya nchi 120, na kuangaliwa LIVE na zaidi ya watazamaji 1bilioni wa Telvisheni na Mitandao ya Interneti.

Miss Tourism 2005
 Tamasha hilo Kuu la Utalii la Dunia “World Great Safari Tour 2014/2015” litajumuisha mashindano ya dunia ya Miss Tourism University World 2014/15,Mbio za nyika za Dunia za Ant Poaching International  Marathon, Wild Life International Marathon, National Parks International Marathon, Mbio za kimataifa za Magari na Baisikeli na tuzo za Dunia za Utalii “World Tourism Awaards 2014/2015”. 

MissTourism 2006
Pia kutakuwa na michezo mbalimbali ya viwanjani,majukwaani ,ufukweni na katika maeneo mengine ya kitalii na utalii ikiwemo masumbwi na kubwa zaidi ni washiriki wote wa kitaifa na kimataifa kushiriki katika Safari kuu ya kitalii ,wakiambatana na waandihi wa habari wa kimataifa na kitaifa wa Televisheni,Video, Majarida na Magazeti katika vivutio vya Utalii,maeneo ya kitamaduni na kihistoria vya  nchi wenyeji.
Miss Tourism 2007


Vigezo ambavyo Bodi intazingatia katika kuteua nchi wenyeji ni pamoja na Uwepo wa Vivutio vya Utalii katika nchi husika, Dhamila na juhudi za nchi husika kutangaza utalii wake kimataifa na kitaifa, Haja,Juhudi,Utayali na dhamira ya kupiga vita Ujangili ,Uharibifu wa Mazingira ya nchi husika katika nchi husika, lakini kubwa zaidi ni Amani,Usalama,Fulsa za Uwekezaji wa kitalii na utengamano wa kimataifa na kitaifa wan chi husika. Pia nchi kuwa na uwezo wa kuwa wenyeji wa tukio au tamasha la kimataifa hapa suala la miundombinu ya mawasiliano,usafiri,mahoteli,rasilimali watu,utayari wa serikali na mamlaka zake za utalii,mazingira katika kushirikiana na waandaaji na mahitaji mengine ya msingi vinazingatiwa.

                        Miss Tourism Tanzania 2011

 


 Miss Tourism 2009
Asante,

Gideon Erasto Chipungahelo
Makamu wa Rais Dunia Africa Tourism Promotion Centre/ Miss Tourism Organisation

No comments: