Miss Tourism World 2005- Africa

Miss Tourism  World 2005- Africa
Africa Tourism Promotion Centre

NGORONGORO CRATER

NGORONGORO CRATER
We Welcome Miss University Tourism World 2014 Contestants to Africa

THE GIDEON

AFRICA TOURISM PROMOTION CENTRE ,KURATIBU MASHINDANO YA MISS UTALII TANZANIA NA MISS TOURISM UNIVERSITY WORLD


Taarifa Kwa Vyobo Vya Habari                         Taraehe 5-8-2017
BODI YA MASHINDANO YA MISS UTALII TANZANIA YATEKELEZA MAAGIZO YA BASATA – CHINI YA AFRICA TOURISM PROMOTION CENTRE
Bodi ya wakurugenzi ya kapuni ya Miss Tourism Tanzania Organisation yenye dhima ya kikomo ya kuandaa ashindano ya Miss Utalii Tanzania na ya Miss Tourism University World, Miss Tourism Tanzania  imeikaimisha kampuni ya Africa Tourism Promotion Centre , kuratibu ashindano ya Miss Utalii Tanzania , ambayo yalisitishwa na Bodi hiyo na BASATA mwaka 2013.

kwa mujibu wa Taarifa iliyo tolewa na Taasisi hiyo na kusainiwa na   mwenyekiti mtendaji wa Africa Tourism Promotion Centre ambaye pia ni rais wa mashindano hayo, amesema kuwa hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa aelekezo ya BASATA na Bodi ya mashindano ilikuiarisha uongozi na mfumo wa mashindano ili kuyaboresha kwa viwango vya kimataifa.

Pamoja na mambo mengine African Tourism Promotion Centre ,itasimamia mashindano hayo kwa  mfumo mpya ambao umepitishwa na bodi,ikiwemo mashindano kufanyika kuanzia ngazi za kanda badala ya wilaya na mikoa, ili kuimalisha ubora na  upatikanaji wa washiriki wenye viwango.

Mashindano ya Miss Utalii Tanzania tofauti na mashindano mengine chini yamekuwa ndiyo pekee yakiiletea heshima na kuitangaza Tanzania kwa kushinda mataji ya kimataifa ndangu kuanzishwa kwake nchini mwaka 2005. Huku yakiwa ni ya kwanza katika historia ya Tanzania kutwaa taji la Dunia, na pia kuipa heshima Tanzania kwa kuwa wenyeji wa fainali za Dunia ambapo mwaka 2006 fainali za dunia za  Miss Touris  World 2006 zilifanyika nchini na kushirikisha nchi zaidi ya 100. Na Mwaka 2005 Tanzania iliingia katika historia ya Dunia ya Tasnia ya urembo kwa kutwaa taji la kwanza la dunia kupitia kwa Miss Utalii Tanzania 2005 -Witness Manwingi, huo ulikuwa ni mwanzo wa mfululizo wa mataji ya kimataifa kila mwaka ambao Miss Utalii Tanzania walishiriki,ikiweo Miss Utalii Tanzania kutwaa mataji ya dunia mwaka 2006 kupitia kwa Miss Utalii Tanzania  2006 -Killi Janga huko China Taipei, 2007 kupitia kwa Miss Utalii Tanzania  2007 - Lilian Siprian huko Uturuki n.k.

Tangu Kusitishwa kwa mashindano ya Miss Utalii Tanzania nchini mwaka 2013, tasnia ya urembo nchini imedorola kabisa na kupoteza msisimko uliokuwepo kabla ya kusitishwa kwa mashindano hayo.

Ni matarajio yetu kwamba ujio mpya wa mashindano Miss Utalii Tanzania, baada ya kukamilisha taratibu zote za BASATA itakuwa ni chachu ya kurudisha msisimko na hadhi ya mashindano ya urembo na mitindo nchini. 

Bodi ya Miss Utalii Tanzania imesikitishwa sana na hali ya kudorola kwa sanaa na tasinia ya urembo na mitindo nchini.

Asante,

Gideon E. Chipungahelo
Mkiti Mtendaji Bodi ya Miss Tourism Tanzania Organisation
No comments: