MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL

MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL
Miss Tourism Tanzania Pageants

Miss Tourism Tanzania Pageant

Miss Tourism Tanzania Pageant
We Welcome Miss Tourism Tanzania Organisation

Miss Tourism World 2005- Africa

MISS TOURISM TANZANIA PAGEANT

WORLD GREAT SAFARI TOUR KUSHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI WA MICHEZO NA BURUDANI

Top Five Miss Tourism Tanzania 2013, Kutoka kushoto ni Asha Ramadhani (Katavi),Lucy Noel(Dar Es Salaam) ,Hadija Saidi (Morogoro)Theresia Kimola,(Vyuo Vikuu) na Mwanakombo Kessy (Singida)
Waandaaji na waratibu wa matamasha ya World Great Safari Tour 2014,Africa Tourism Promotion Centre ,wameboresha zaidi Tamsha hilo kwa kuongeza idadi ya aina ya matukio yanayo jumuisha tamasha hilo la Dunia. Hivyo kufanya World Great Safari Tour liwe ni Tukio linalo jumuisha mashindano ya Dunia ya Miss University Tourism world 2014,Ant Poaching International Marathon 2014,World Tourism Worlds 2014, World Great Safari Motor Rally 2014, Wildlife International Marathon 2014, World Great Safari Cycling 2014, World Great Tourism ,Antipoaching and Environment Protection Conferance 2014. Hili ni tukio kubwa la kitalii Duniani na Afrika ambapo Waandishi wa habari watajumuika  na Wanamichezo ,Wanamitindo ,na wasanii wa kitaifa na kimataifa  utembelea na kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania huku wakipiga picha za Matangazo ya Video, Majarida, Magazeti na Televisheni.


Miss Utalii Tanzania 2013 , Hadija Said (Katikati) , Mshindi wa Pili Lucy Noel ( Kushoto) na Mshindi wa Tatu Theresia Kimolo (Kulia)
World Great Safari Tour 2014,ni tukio kubwa la kitali kuwahi kufanyika Africa, ambalo litajumuisha mashindano ya Dunia ya Miss University Tourism World 2014, Tuzo za Dunia za World Tourism Award 2014, mashindano ya Dunia ya mbio za Nyika za Ant Poaching International Marathon 2014, Wildlife International Marathon 2014 na National Parks International Marathon 2014, sambamba na World Great Safari Tour 2014. Tukio la World Great Safari Tour 2014,ni fulsa na heshima ya pekee kwa bara la Afrika ,hususani nchi itakayo teuliwa kuwa wenyeji wa Mashindano hayo , kutangaza vivutio vyake vya Utalii kitaifa na kimataifa ,lakini pia kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili na uharibifu wa Mazingira. Matukio yote ya World Great Safari Tour 2014 , yakiwemo ya Mbio za Kimataifa za Magari,Baiskeli na Pikipiki yatalushwa LIVE duniani kote kupitia Televisheni na Internet,moja kwa moja kutoka nchi wenyeji Barani Afrika. Inakadiliwa watazamaji zaidi ya Bilioni 1 watashudia moja kwa moja matukio haya.

World Great Safari Tour 2014,inaratibiwa na kampuni ya kimataifa ya Africa Tourism Promotion Centre (ATPC)


No comments: