Fainali za Dunia za Miss
Utalii 2013 (Miss Tourism World 2013),zitafanyika nchini Equatorial Guinea,
trehe 2 ,Oktoba 2013. Fainali za Dunia mwaka huu zitashirikisha zaidi ya nchi 100 kutoa dunia nzima ikiwemo
Tanzania.
Katika fainali hizo za Dunia
ambazo Tanzania itakuwa inashiriki kwa mara ya tano ,itawakilishwa na mshindi
wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Saidi Juma (Pichani),
ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2013. Hadija Saidi Juma, ambaye
alitwaa taji la Taifa baada ya kuwashinda warembo wengine 29 kutoka mikoa yote
ya Tanzania na Vyuo Vikuu katika fainali za Taifa , zilizo fanyika tarehe
9-5-2013 katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, ataondoka nchini tarehe
28-10-2013.
Miss Utalii Tanzania
imeijengea heshima kubwa Tanzania, sio kwa kuwa ya kwanza kutwaa taji la duni
nchini tu,bali pia kwa kushinda mataji katika fainali zote za dunia tulizo
shiriki, ambapo hadi sasa tunashikilia mataji manne ya Dunia. Mataji hayo na
nchi yaliko fanyika katika mabano ni pamoja na Miss Tourism World 2005 –Africa
(Zimbabwe), Miss Tourism World 2006 – SADEC (China Taipei), Miss Tourism Model
Of The World 2006 – Personality (Tanzania), Miss Tourism World 2007 – Africa
(Uturuki), Miss Africa 2006- 1st Runner Up na Miss Freedom Of The World 2013-
Model.
Maandalizi ya kumwandaa Miss
Utalii Tanzania 2013, kwaajili ya kushinda taji la dunia,yanaendelea vizuri
,ili aweze kulinda heshima ya Tanzania na kuvuka rekodi ya warembo
waliotangulia yanaendelea vizuri. Ambapo ili kuhakikisha ushiriki wake katika
mashindano hayo ya dunia unakuwa na manufaa ya kutangaza Utalii wa Tanzania
kimataifa, tumesha peleka maombi maalum Katika mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
na mamlaka ya Hifadhi za Taifa ziweze kudhamini ushiriki huo na kufanikisha
zaidi maandalizi.
Tofauti na mashindano
mengine, washiriki wote wa fainali hizo za dunia watapewa fulsa maalum ya
kutangaza utalii na utamaduni wan chi zao kupetia vyombo mbalimbali vya habari duniani,
jukwaani na nje ya jukwaa.Hii itkuwa ni fulsa nyingine ya pekee kwa
Tanzania,TANAPA na Ngorongoro Crater kutangaza Hifadhi na vivutio vya utalii
vya Tanzania kimataifa, kupitia Miss Utalii Tanzania 2013 katika mashindano
hayo.
No comments:
Post a Comment