Miss Tourism World 2005- Africa

Miss Tourism  World 2005- Africa
Africa Tourism Promotion Centre

NGORONGORO CRATER

NGORONGORO CRATER
We Welcome Miss University Tourism World 2014 Contestants to Africa

THE GIDEON

Miss Utalii waipongeza Eriado Point View

MKURUGENZI wa Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Dar es Salaam, Jomo Malyaga, ameumwagia sifa Ukumbi wa Eriado Point View, kwa kuliunga mkono shindano hilo linalotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.


Maandalizi ya Miss Utalii Vyuo Vikuu kwa sasa yanaendelea jijini Dar es Salaam, huku likipangwa 
kufanyika katika ukumbi huo uliopo Pugu. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Malyaga alisema Eriado ni mdhamini wa kwanza kujitokeza katika shindano hilo, linalosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mambo ya urembo hapa nchini.


Alisema wanaamini kwa kuungwa mkono na wadau, wakiwamo hao wa Eriado, mambo yatakuwa mazuri, huku shindano hilo likifanyika kwa ufanisi. “Nia ni kufanya shindano kubwa na lenye mafanikio, hivyo tunashukuru kwa dhati kwa kuanza kuungwa mkono na wenzetu wa Eriado, walioamua kulipeleka kwenye ukumbi wao.


“Naamini mambo yatakuwa mazuri, hivyo wadau na mashabiki waendelee kusubiri, ukizingatia tumejipanga kuwaletea shindano lenye ubora wa hali ya juu,” alisema. Miss Utalii ni miongoni mwa sekta za urembo zenye mafanikio makubwa hapa nchini, hasa kutokana na warembo wake kufanya vyema katika shindano la Dunia.
Chanzo: Jiachie Blog

No comments: