MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL

MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL
Miss Tourism Tanzania Pageants

Miss Tourism Tanzania Pageant

Miss Tourism Tanzania Pageant
We Welcome Miss Tourism Tanzania Organisation

Miss Tourism World 2005- Africa

MISS TOURISM TANZANIA PAGEANT

BODI MISS UTALII YATANGAZA NAFASI ZA MAWAKALA


BODI YA MASHINDANO MISS UTALII TANZANIA YATHIBITISHA MAWAKALA, NAKUTANGAZA NAFASI ZA UWAKALA 2011/2012
Bodi ya Taifa ya mashindano ya Miss Utalii,katika kutekeleza mkakati wake wa kujiimarisha na kujipanga kwa ajili ya mpango mkakati mpya wa muda mfupi na muda mrefu wa miaka mitano na wa miaka kumi,imethibitisha waandaaki wa mashindano hayo katika  mikoa na kanda 17, huku ikitangaza nafasi za wandaaji katika mikoaa na kanda mbalimbali Tanzania bara na Tanzania Visiwani.
Katika kupitisha makampuni na majina ya waandaaji hao wa ngazi za mikoa, bodi imezingatia uwezo ,umakini na uwepo wa ofisi na waandaaji katika wilaya,mikoa na kanda husika. Pia bodi imezingatia kuwa na waandaaji makini ambao wanaweza kuendana na mfumi mpya wa kitaasisi wa mashindano haya, mfumo ambao unatoa fulsa ya mgawanyo wa madaraka na uwajibikaji wa pamoja na kila mmoja katika ngazi yake. “ Bodi sasa imeamua kujenga taasisi imara ya kiheshimika na kukubalika kitaifa na kimataifa,ni wakati sahihi sasa kwa mashindano haya kuchukua nafasi yake ya kuwa shindano bora na kubwa kuliko yote nchini,Afrika na duniani kwa ujumla, na hili litawezekana tu kwa kuwa na taasisi imara na makini iliyojengwa na watu na makampuni  makini. Wale waandaaji wababaishaji,mamluki na wahuni sasa Miss utalii Tanzania sio mahala pake”. Aidha bodi imewataka wasandaaji wote kukamilisha taratibu na matakwa ya kanuni na taratibu za mashindano haya,kabla ya kufanya kwa mashindano ya ngazi zao,ikiwemo kwenda kujitambulisha na kuchukua vibali vya maafisa utamaduni. Aidha bodi imewaomba maafisa utamaduni wa ngazi zote kutotoa vibadi kwa waandaaji hao kabla ya kukamilisha taratibu iliwemo kukabidhi zawadi za washindi na washiriki siku saba kabla ya tarehe za shindano husika.
Mikoa na kanda hizo na majina ya waandaaki katika mabano ni Arusha,Mara na Kanda ya Kaskazini ( NAman LIMITED COMPANY LTD), Kilimanjaro na Manyara (NEW VISION PLAN COMPANY LTD),Kagera ( FIOONA FASHION Limited) Mbeya ( WABUNIFU ENTERTAINMENT), katavi ( KATABI COMPANY LIMITED), Dar es Salaam,Kinondoni,Ilala na Temeke ( Tanzania Film Directors Association (TAFIDA)) Vyuo Vikuu Dar es Salaam (Eriado Point View) ,Iringa na Kanda ya Kusini (DELIMA Hotel & Tourism School),Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki ( L.J MEDIA COMPANY), Mwanza (Fania Beauty and Salon Company).
Mikoa ambayo haijapata waandaaji baada ya maombi ya waliotuma kutikuwa na sifa, hivyo wenye sifa wajitokeze kuomba kuandaa ni : Njombe, Pwani,  Lindi, Mtwara, Tanga Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora, Rukwa, Kigoma, Kanda ya Kati, Kanda ya Mashariki, Zanzibar, Kanda ya Kusini Nyanda ya Juu, Kanda ya Magharibi, ,Vyuo Vikuu Kusini,Vyuo Vikuu kaskazini,Vyuo Vikuu Magharibi,Vyuo Vukuu Kati,na Vyuo Vikuu.
Makampuni na watu wanaotaka kuandaa mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania wawasiliane nasi kupitia barua pepe ya missutaliitanzania@gmail.com ,ukurasa wetu wa facebook wa miss tourism/missutalii tanzania na au ofisi za vyombo mabalimbali za vyombo vya habari. Fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012, sasa zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe za uhuru 8/12/2012 baada ya kuahitishwa kupisha utaratibu na kalenda mpya ambapo sasa kila mwaka Fainali za taofa zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe za uhuru. Mikoa na kanda zote zinatakiwa kuwa zimekamilisha fainali zake kabla ya Novemba 15 kila mwaka.
Asante,
Frances Samwel Mwella
Mkitugenzi wa mashinfano ya Ngazi za Wilaya,Mikoa na Kanda

No comments: