MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL

MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL
Miss Tourism Tanzania Pageants

Miss Tourism Tanzania Pageant

Miss Tourism Tanzania Pageant
We Welcome Miss Tourism Tanzania Organisation

Miss Tourism World 2005- Africa

MISS TOURISM TANZANIA PAGEANT

MIKIDADI MAHMOID MWENYEKITI BODO MISS ITALII



MIKIDADI MAHMOUD MWENYEKITI WA BODI MISS UTALII TANZANIA
Bodi ya Miss Tourism Tanzania Organisation,yenye dhima ya kikomo ya kuaandaa na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania ,imemteua Ndugu Mikidadi Mahamoud kuwa mwenyeketi ya bodi ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania. Uteuzi huo utakuwa ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 1-10-2012.

Akuthibitisha uteuzi huo, Gideon Chipungahelo,Rais wa Miss Utalii Tanzania, hatua hii ni moja ya utekelezaji mpango mkakaeu wa miaka mitano wa kuimalisha mashindano na mfumo wa uongozi wa mashindano haya. Ambapo sasa tunakuwa na bodi ya mashindano na bodi ya taifa ya ushauri ambayo itajumuisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na serikali. Tayali tumeiandikia serikali kupitia Bodi ya Utalii Tanzania, tukiiomba kuwa na wajumbe katika bodi ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania, ambapo kutakuwa na wajumbe pia kutika katika mamlaka mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Mazingira, Elimu, Afya, Uwekezaji, Jinsia na asasi za kupambana na umasikini kupitia utalii na utamaduni. Mamlaka na Asasi hizo ni pamoja na Mamlaka za Hifadhi za Taifa, Bodi ya Utalii, Bodi ya Madini, Kurugenzi ya Utamaduni, Kurugenzi ya Utalii, Kituo cha uwekezaji Tanzania, Kurugenzi ya Mazingira na Tanzania Association for Tour operators.
Lengo la kufanyia mabadiliko ya mfumo wa uongozi na uendeshaji ni pamoja na kupanua wigo wa ushiriki wa mamlaka za umma na za binafsi katika uendeshaji wa mashindano haya,ambayo hakika ni alama ya urithi wa taifa na muhimu sana katika kuhamasisha ukuaji wa utalii wa Tanzania na kuhamasisha Utalii wa ndani,utalii wa kitamaduni,utumiaji wa bidhaa za kitanzania,utalii wa michezo,utalii wa mikitano,pia kuhamasisha vita dhidi ya uharibifu wa mazingira,uwundaji haramu,uvuvi haramu,tamaduni kongwe na potofu,vita dhidi ya ujinga,umasikini na maradhi.
Bodi katika kumteua Ndugu Mikidadi Mahamoud kuwa mwenyekiti wa bodi,imezingatia busara,hekima na uzoefu wake mkubwa katika katika Nyanja za kitaifa na kimataifa za michezo,utangazaji,uhamasishaji na ushiriki wake mkubwa katika kufanikisha matukio makubwa ya Kitaifa na kimataifa.Tunaamini uzoefu na uimara wake mkubwa katika uongozi wa kada mbalimbali utakuwa ni muhimili na chachu mpya ya mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania na kuchangia katika ukuaji wa sekta ya Utalii nchini. Mikidadi Mahaumod ambaye amewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa na kimataifa, kwa sasa ni Mkurugenzi wa Redio uhuru ya jijini.
Aidha fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania kuanzia mwaka zitakuwa zikifanyika mwezi Didemba 2012 sambamba na sherehe za Uhuru wa Tanzania . Ambapo kwa mwaka huu, karibu mikoa yote imekamilisha fainali zake, kasoro mikoa ya Arusha,Dodoma,Kulimanjaro,Mara na Iringa ambayo warembo wapo kambini wakiendelea na mazoezi na itakuwa imekamilisha fainali hizo kabla ya Novemba 15 ,2012.




No comments: