MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL

MISS TOURISM TANZANIA INTERNATIONAL
Miss Tourism Tanzania Pageants

Miss Tourism Tanzania Pageant

Miss Tourism Tanzania Pageant
We Welcome Miss Tourism Tanzania Organisation

Miss Tourism World 2005- Africa

MISS TOURISM TANZANIA PAGEANT

MATUKIO NA VIJANA: MTOTO WA MBUNGE ALIYETWAA MISS TANZANIA APINGWA

MATUKIO NA VIJANA: MTOTO WA MBUNGE ALIYETWAA MISS TANZANIA APINGWA



 Tatizo la Tanzania,ni kutokuwa na wataalaam wa sanaa ya urembo katika ngazi zote binafsi na za umma,na hata katika mamlaka husika.Mbaya zaidi hata wale wachache tuliobahatika kuwa nayo tunapigwa vita badala ya kujifunza kutoka kwetu.Sanaa ni nyanja pana kama ulivyo udaktari , kuna daktari wa macho,mifupa,tumbo,uzazi,kichwa n.k.



hivyo taaluma ya sanaa ya urembo ina utaalaam wake na kanuni zake kuu kimataifa, ambazo tukiziikwepa na kuingiza za kivyetu vyetu matokeo yake ndo hayo. Tunaingiza siasa katika sanaa ambayo inamiiko,kanuni na taratibu zake kimataifa.



Wakati sasa umefika,kwa watanzania na mamlaka husika za sanaa kutoa fusa kwa wabunifu na waratibu wa sanaa ya urembo watekeleze na waendeshe sanaa hiyo bila ya kuingiliwa na mamlaka hizo wala watanzania kwa ujumla. Kipimo kiwe ni mafanikio kimataifa na utekelezaji wa majukumu ya mshindi kwa Taifa.



Wengi wanao kosoa washindi + matokeo hawajui sifa za washindi,taratibu na hata kanuni za mashindano husika kitaifa wala kimataifa umpata mshindi wa shindano la urembo ni hatua ndefu ambayo huanzia siku ya kwanza mshiriki anaporipoti kambini, hakuna hata shindano moja duniani ambalo mshindi hupatikana jukwaani siku ya mwisho.



SANAA YA UREMBO INAKUFA NA INAUAWA NA MFUMO WA USIMAMIZI ULIOVULUGWA BAADA YA MIAKA 2006, HAKUNA TENA MIPAKA NA MGAWANYO WA MAJUKUMU BAINA YA WAANDAAJI NA WASIMAMIZI. NASHAURI MAMLAKA HUSIKA KUKAA NA WAANDAAJI ILI KUNUSURU SANAA UREMBO NCHINI,BADALA YA KUTEGEMEA MAJUNGU NA FITINA

No comments: