Miss Tourism World 2005- Africa

Miss Tourism  World 2005- Africa
Africa Tourism Promotion Centre

NGORONGORO CRATER

NGORONGORO CRATER
We Welcome Miss University Tourism World 2014 Contestants to Africa

THE GIDEON

WORLD GREAT SAFARI TOUR FESTIVAL 2015WORLD GREAT SAFARI TOUR FESTIVAL 2015
World Great Safari Tour Festval,ni tukio kubwa la kitalii Duniani kuwahi kufanyika barani Africa. World Great Safari Tour Festival linajumuisha matukio ya kimataifa ya Michezo,Utamaduni,Burudani na Utalii ikiwemo :Miss Tourism University World 2015, World Tourism Award 2015, Ant Poaching International Marathon 2015, Wildlife International Marathon 2015 na National Parks International Marathon 2015 na ,World Great Safari Rally 2015.


Hii ni fulsa na heshima ya pekee kwa nchi wenyeji na bara la Afrika , kutangaza vivutio vya Utalii, Mianya ya Uwekezaji, kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili na uharibifu wa Mazingira. Lakini pia ni fulsa kwa serikali na mamlaka za nchi mwenyeji kuidhihirishia dunia jitihada inazochukua na mafanikio yake ya vita dhidi ya Ujangili, hasa Uwindaji haramu,na Uharibifu wa Mazingira.Ni fulsa pia kwa sekta binafsi kukuza na kupanua biashara yake kwa kupenyeza bidhaa zake katika soko la kimataifa kwa kujitangaza kupitia tamasha hili adhimu duniani.

Matukio yote ya World Great Safari Tour Festival 2015 yatarushwa LIVE kupitia Televisheni na Mitandao ya Internet duniani. Vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa na kitaifa vikiripoti matukio ya kilasiku na uwepo katika nchi wenyeji wa zaidi ya washiriki 1200 kutoka nchi zaidi ya 100 duniani kote, wakiomo watu mashuhuri na maarufu Duniani kupitia Televisheni na Internet,moja kwa moja kutoka nchi wenyeji Barani Afrika.

Inakadiriwa kwamba Uwepo wa wageni wa kimataifa 2500, ikijumuisha washiriki 1200, waandishi wa habari wa kimataifa 200, viongozi 100 wasindikizaji, ndugu, jamaa na marafiki 1000.Kutazalisha sio chini ya Dola za Marekani 500,000 kila siku  na Dola 10,000,000 kwa siku 20 za Tamasha hilo, ikiwa ni matumizi ya kadirio la chini la kila mmoja dola 200 kwa siku.

Zaidi ya watazamaji Bilioni 1 wa televisheni na mitandao ya Internet Duniani kote watashudia LIVE, huku zaidi ya wafuatiliaji zaidi ya 1.5 Bilioni wakisoma, kufuatilia na kuangalia kupitia taarifa mbalimbali za vyombo vya habari vya Televisheni, Mitandao ya Internet, Majarida na Magazeti kila siku ,wakati wote na baada ya World Great Safari Tour Festival 2015.World Great Safari Tour Festval 2015, inaratibiwa na Africa Tourism Promotion Centre (ATPC).

No comments: